Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea apata dhamana, kuendelea na kampeni Kinondoni
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea apata dhamana, kuendelea na kampeni Kinondoni

Saed Kubenea
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha nchini Tanzania, imemwachia kwa dhamana mgombea ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo, Saed Ahmed Kubenea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kubenea ambaye alikuwa mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam kupitia Chadema, ameachiwa leo Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 baada ya kukamilisha masharti ya dhama katika kesi inayomkabili.

Jumatatu tarehe 7 Septemba 2020, Kubenea alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kwa makosa mawili la kuingia nchini Tanzania akitokea Kenya kinyume na Sheria ya Uhamiaji, Sura ya 54 Marejeo ya mwaka 2016.

Pia, anatuhumiwa kuingiza nchini fedha za kigeni bila kutoa tamko kinyume na Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha Mpakani za mwaka 2016.

Kiasi anachotuhumiwa kuingiza ni Sh.29 milioni ambazo ziko katika mchanganuo wa fedha za Kenya Sh.491,700, Dola za Marekani 8,000 na Sh.71,000.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi tarehe 21 Septemba 2020.

Baada ya kutoka mahakamani, chama chake cha ACT-Wazalendo ambacho kilimpitisha kugombea ubunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumteua kugombea ubunge Kinondoni jijini Dar es Salaam, kimewaka Wanakinondoni kujiandaa kwa uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa na Janeth Rithe, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma imesema, ACT-Wazalendo kimewapongeza kwa dhati mawakili waliofanikisha hatua ya mgombea wao kupata dhamana wakiongozwa na Sheki Mfinanga na Alute Mughwai.

“Tunawashukuru wanachama, wapenzi na mashabiki wa ACT- Wazalendo kwa kututia moyo kwa njia mbalimbali ikiwamo ya maombi na sala na hatimaye mgombea wetu kupata dhamana.”

“Baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, tunawasihi wanachama, wapenzi na wapiga kura wetu wa Jimbo la Kinondoni kufuatilia ratiba ya mikutano ya kampeni ya Saed Kubenea ili wakasikilize sera na ahadi zilizomo kwenye Ilani ya ACT-Wazalendo kwa jimbo hilo na Taifa kwa ujumla,” amesema Janeth

Janeth amesema, Kubenea anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari katika siku za karibuni juu ya suala hili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!