Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yamkingia kifua Rais Samia sakata la bandari
Habari za Siasa

CCM yamkingia kifua Rais Samia sakata la bandari

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mpango wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kutafuta mwekezaji binafsi wa kuendesha bandari nchini, ni utekelezaji wa ilani yake na kwamba hata kama angekuwa kiongozi mwingine angefanya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida…(endelea).

Hayo yamelezwa jana tarehe 23 Julai 2023 na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Singida, akiwajibu wapinzani wanaopinga mpango huo kwa madai kuwa hauna tija.

Serikali ya Rais Samia, kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imeingia mkataba wa ushirikiano wa kiserikali na Serikali ya Dubai, kupitia kampuni yake ya Dubai Port Wolrd, kwa ajili ya kuendesha, kuendeleza na kusimamia bandari hususan bandari ya Dar es Salaam.

Katibu mkuu huyo wa CCM, amesema chama chake kimebariki uamuzi huo baada ya kuchambua na kujiridhisha kwamba una tija kwa Taifa.

“Tunachofanya sasa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi, hata angekuwa nani angetekeleza ilani na sera za chama. Ilani imeandikwa wakati huo mwenyekiti wa CCM alikuwa Hayati John Magufuli, leo amekuja Rais Samia amechukua kiti na shurti aendeleze yote yenye tija,” alisema Chongolo.

Chongolo alisema, Serikali imetoa wito kwa watu wenye maoni juu ya maboresho ya mkataba huo kuwasilisha ili yafanyiwe kazi, hivyo wanaopinga wanapaswa kutumia nafasi hiyo.

“Kuna watu wanasema jambo hili la Rais Samia, wala sio la Serikali au la chama, naomba niwaambie mtu mwenye akili akija kuwaambia jambo la hovyo maana yake nini? Kazi ya watu wanaotafuta dola kututoa madaraka, ni kutengeneza mazingira ya kutugombanisha na watu waliotupa dhamana ya nchi. Sisi tunawajua kuliko wanavyojijua na wala hatutumii nguvu tunawaacha wahangaike,” alisema Chongolo.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, akizungumza mkoani Dodoma, aliwataka wananchi wampe nafasi Rais Samia kutekeleza yale anayokusudia kufanya chini ya ilani ya chama hicho.

“Lazima tumpe mtu nafasi yale aliyokusudia chini ya CCM yatimie, ikifika 2025 tunakwenda na Rais Samia, “Kwa hali ilivyo na kwa hatua tuliyopiga tukienda hivi mpaka kufika 2025 mimi nina uhakika kila Mtanzania atakuwa na sababu ya kusema tuendelee na CCM, tuendelee na Rais Samia,” alisema Kinana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!