Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yaiagiza Serikali kusikiliza ushauri wa wananchi kuhusu tozo
Habari za SiasaTangulizi

CCM yaiagiza Serikali kusikiliza ushauri wa wananchi kuhusu tozo

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

 

KAMATI Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM imeiagiza serikali kusikiliza maoni na ushauri wa wananchi kuhusu utekezaji wa bajeti ya 2022/2023 hususani eneo la tozo za miamala ya kielektroniki iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni.

Pia imeiagiza serikali kubana matumizi na kuendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi ya biashara ili kujenga uchumi imara unaozalisha kwa lengo la kutanua wigo wa kodi na vyanzo vya kodi vyenye mifumo rafiki kwa kila mmoja. Anaripoti Erick Mbawala, TUDARCo … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 8 Septemba, 2022 jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu yaliyojiri katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM iliyoketi juzi jijini Dar es Salaam.

Shaka amesema kamati kuu hiyo iliyoketi chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, ilipokea, kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu hatua za kibajeti zinazoendelea kuchukuliwa kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kasi, eneo mojawapo ni kupitia tozo.

Amesema serikali imefanya mambo kadhaa katika kipindi kifupi ikiwamo ujenzi wa vituo vya afya 234, ujenzi wa sekondari 214 na maeneo mengine ambayo yanagusa maisha ya watanzania kila siku.

“Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM imeielekeza serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maoni na ushauri wa wananchi kuhusu tozo. Maelekezo hayo ya kamati kuu yamezingatia ibara ya 20 (b) ya ilani ya uchaguzi 2025,” amesema.

Aidha, Shaka amesema kamati kuu hiyo ilipokea taarifa ya maendeleo ya mchakayto wa kuwapata wabuge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

“Chama kinaendelea na utaratibu wa ndani ambapo utaratibu utakapokamilika chama kitatoa taarifa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amesema chama hicho, kinafuatilia kwa karibu mienendo na uwajibikaji wa wateule wa rais aliowapa dhamana ili kuona wanatimiza lengo ambalo rais alitamani kuona wakati anawapa dhamana hizo.

1 Comment

  • Lakini waliopitisha sheria ya tozo si ni wale wale wa kamati kuu? Rais, spika, mawaziri nk Mkono wa kulia unapitisha na mkono wa shoto unapinga. Tuache unafiki
    Mumeshindwa kukusanya kodi ya mapato kutoka mabilionea na sasa mnawakamua wavuja jasho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!