Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Bunge Tanzania lazoa makombe 7, Majaliwa awapongeza
Michezo

Bunge Tanzania lazoa makombe 7, Majaliwa awapongeza

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameipongeza timu ya Bunge la nchi hiyo, baada ya kuibuka na makombe saba katika michezo mbalimbali kwenye Mashindano ya 11 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyomalizika hivi karibuni jijini Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Amesema wabunge hao wamefanya kazi kubwa ya kuipambania Tanzania na Bunge la Tanzania mbele ya nchi zote za Afrika Mashariki.

“Ile kazi nzuri mliyoifanya ya kuipambania nchi, mmeleta zawadi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania na wabunge wengine,” alisema Majaliwa

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana Jumamosi, tarehe 18 Desemba 2021, alipozipokea timu mbalimbali za Bunge katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Timu ya Bunge imeshinda makombe kwenye michezo ya mpira wa miguu, pete, wavu kwa wanawake na wanaume, kikapu kwa wanawake na wanaume na mchezo wa kuvuta kamba wanaume.

“Ninaleta kwenu salamu za faraja kutoka kwa Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa mliyoifanya, na faraja nyingine ni kuona wachezaji wengi mmerudi salama, nidhamu mlioionesha katika mashindano haya imetujengea heshima kubwa,” alisema.

Alisema ushindi wa timu hiyo unapeleka ujumbe kwenye timu nyingine zinazoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa kushiriki kikamilifu na kuiwakilisha vyema nchi kwenye mashindano husika ikiwemo kuwa na matamanio ya kurudi na makombe.

“Tunatakiwa tuandike historia ya ubora wa michezo nchini ambapo tunaona kwasasa kila sekta inaenda vizuri na hata ile inayokuwa inakufa tunaifufua na hii pia imepelekea kupata heshima na sifa ya kupeleka timu yetu ya watu wenye ulemavu kwenye mashindano ya kombe la dunia”

Kwa upange wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema kupitia michezo hiyo wametoa somo kwa timu nyingine zilizoshiriki michezo hiyo na hatimaye kulipa heshima bunge “ahadi yetu sisi tutasimama na ninyi kwenye maandalizi zaidi mwakani na ninawapongeza sana kwa nidhamu mlioionesha hata mlipochokozwa hamkuchokozeka”

Naye, Meneja wa Timu hiyo, Seif Gulamali alimshukuru Spika Ndugai kwa kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri kwenye mashindano hayo jambo lililowezesha kuibua morali na hatimaye kuibuka na makombe “kwa niaba ya wabunge wote tunaomba usituchoke sisi ni vijana wako, endelea kutulea, tunapoleta maombi yetu basi uyapokee kwa mikono miwili.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!