January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 1.2 wapata chanjo Tanzania, maambukizi yashika kasi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema, maambukizi ya virusi vya korona (UVIKO-19), yanaendelea kwa kasi nchini humo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Imesema, sharti wananchi waepuke mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kunawa mikono na maji tiririka kwa sababu pamoja na kuvaa barako.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jumapili tarehe 19 Desemba 2021, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi amesema, katika kipindi hiki cha likizo, wazazi tuwaepushe watoto kwenda kwenye sehemu zenye mikusanyiko isiyo ya lazima ili kuwalinde watoto.

“Pamoja na kuongezeka kwa Mafua ya Kawaida (Seasonal Influenza) bado tuna visa vya UVIKO-19 na vinaongezeka kwa Kasi, nawaomba wananchi waendelee kuchukua tahadhari zote za Kinga zikiwemo, kunawa Mikono kwa majitiririka, Kuvaa barakoa na kuchanja,” amesema Profesa Makubi

Amesema “familia zinazosafiri kwa ajili ya sikukuu za mwisho mwaka hakikisheni mnawalinda wazee huko vijijini kwa kuchukua tahadhari zote pamoja na kuvaa Barakoa na kuchanja.”

Profesa Makubi amesema, tangu chanjo ya corona ilipoanza kutolewa tarehe 23 Julai 2021 ya Jenssen, Sinopharm na Pfizer hadi kufikia jana Jumamosi tarehe 18 Desemba 2021, wananchi milioni 1.27 sawa na asilimia 2.21 wamepata chanjo kamili. Lengo likiwa kufikia asilimia 60% ya wananchi wote.

Rais Samia Suluhu Hassan akichanjwa chanjo ya korona

Lengo la mkutano huo na waandishi wa habari, lilikuwa kuzungumzia uzinduzi wa Mpango Shirikishi na Harakishi awamu ya Pili dhidi ya UVIKO-19 nchini Tanzania, utakaofanyika tarehe 22 Desemba 2021, jijini Arusha.

Amesema, Mpango Shirikishi na Harakishi awamu ya pili dhidi ya afua za kinga za kinga UVIKO-19, zinaelekezwa timu za afya katika halmashauri na mikoa kuendelea kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kuendelea kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya hatua mbalimbali za kujikinga na UVIKO – 19 ikiwa ni pamoja matumizi ya chanjo.

Profesa Makubi amesema, lengo la Serikali ni kushirikiana wananchi wenyewe na na wadau wa maendeleo kuongeza chachu kwa watoa huduma ngazi ya Jamii kuendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuendelea kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kupata chanjo kwa kufuata maelekezo ya wataalam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi akizungumza na waandishi wa habari

Amebainisha baadhi ya mambo yatakayozingatiwa; ni kuwezesha serikali za mitaa, vitongoji zenyewe kulisimamia zoezi hili la elimu na utoaji wa chanjo na liwe endelevu (kampeni ya mtaa kwa mtaa na kitongoji kwa kitongoji.

“Kuendelea kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ili waendelee kutoa huduma ya chanjo kulingana na Miongozo ya nchi na Shirika la Afya Duniani,” amesema

Amesema, waganga wa wakuu wa mikoa na halmashauri kuongeza vituo vya kutolea huduma za chanjo kulingana na mahitaji, zikiwemo huduma mkoba na kufungua vituo zaidi katika maeeeo ya mikusanyiko.

“Kuendelee kuwatumia watu maarufu kama Viongozi wa Dini, wasanii wanasiasa, wanajamii, wananzengo, wanahabari na viongozi/wazee wa kimila katika mapambano dhidi ya UVIKO – 19,” amesema.

error: Content is protected !!