KAMATI ta Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeishauri Serikali kuimarisha sekta ya habari na mawasiliano, kwa kuwa ni chachu ya maendeleo ya uchumi wa nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Wito huo umetolewa leo Ijumaa, tarehe 20 Mei 2022 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne Kilango Malecela, akiwasilisha maoni na ushauri wa kamati hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya HJabari kwa mwaka 2022/23.
Malecela amesema, kamati hiyo inaishauri Serikali itoe fedha za kutosha kufanikisha mradi wa Anwani za Makazi na Postikodi.
Mbali na wito huo, kamati hiyo imeishauri Serikali isimamie Shirika la Posta (TPC), lipate mikopo ili liweze kulipa madeni inayodaiwa kiasi cha Sh. 26.8 bilioni. Pia, imeshauri taasisi za Serikali zinazodaiwa na shirika hilo, zilipe madeni ili liweze kujiendesha.
Katika hatua nyingine, Malecela amesema kamati hiyo inaishauri Serikali kuliwezesha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), ili zijiendeshe kibiashara kwa kuansiha miradi ya maendeleo.
“Serikali ihakikishe taasisi zake zinalipa madeni ya mashirika haya mfano, deni la TSN limefikia Sh. bilioni 11,” amesema Malecela.
https://www.youtube.com/watch?v=ZWV-O136fo0
Leave a comment