Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge lagoma kurekebisha sheria kuwezesha uwekezaji bandarini
Habari za SiasaTangulizi

Bunge lagoma kurekebisha sheria kuwezesha uwekezaji bandarini

Bunge
Spread the love

BUNGE limegoma kufanyia kazi muswada uliowasilishwa na Serikali kwa ajili ya kurekebisha sheria zinazosimamia rasilimali na maliasili za nchi, uliolenga kuwezesha uwekezaji bandarini, baada ya baadhi ya wadau kuupinga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Agosti 2023, bungeni jiji Dodoma na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, kuhusu muswada huo uliolenga kufanyia marekebisho Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya 2017 na Sheria ya Majadiliano Kuhusu masharti Hasi katika Masiliasili ya nchi ya 2017.

Kiongozi huyo wa Bunge ameeleza kuwa, uamuzi huo umelenga kufanyia kazi maoni yaliyotolewa na wadau kuhusu marekebisho hayo na kwamba Serikali imekubali uamuzi huo.

“Nalazimika kusema neno moja na limekuwa likisemwa huko nje na wadau mbalimbali, ikiwa pamoja na baadhi ya waliokuja kwenye kamati na wengine walitoa maoni yao kwa njia ya maandishi na kwa hivyo wafahamu kwamba maoni yao yamefanyiwa kazi kwa sehemu kubwa,”

“Pia, maeneo yalikuwa yakizungumzwa sana huko nje, kuhusu mabadiliko ambayo yangekuwa kwa sehemu ya nne na tano kwenye muswada ule wa marekebisho ya sheria mbalimbali, kwa maana ya mabadiliko yaliyokuwa yanapendekezwa kwenye sheria yetu ya maliasili,” amesema Spika Tulia na kuongeza:

“Marekebisho ambayo yalikuwa yanapendekezwa kwenye sheria yetu ya rasilimali Bunge halijayakubali, kwa hivyo hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika katika sheria hizo. Kwa hivyo ni muhimu niliseme hilo sababu pamoja na marekebisho mengine limezungumzwa sana na wadau huko nje kwa hiyo Bunge limefanyia kazi maoni yao na Serikali imekubaliana na Bunge katika zoezi hilo.”

Miongoni mwa watu waliopinga marekebisho ya sheria hizo ni Balozi Wilbroad Silaa, aliyedai kuwa yalilenga kupora uhuru wa wananchi kumiliki rasilimali zao, akisema kwamba kifungu cha 38 (2)(a) na (b) cha marekebisho hayo, kilichopendekeza masuala yanayohusu rasilimali kujadiliwa bungeni badala yake yajadiliwe katika Baraza la Mawaziri.

Balozi Slaa alidai kuwa, mapendekezo hayo kama yangefanyika, masuala ya rasilimali za taifa yangejadiliwa katika baraza hilo ambalo halina makali kisheria ya kumlazimisha Rais kutekeleza mapendekezo yake.

“Sasa naomba niwaonye vitu viwili, katiba yetu inasema nini? Baraza la Mawaziri ni chombo cha kushauri, kwa hiyo kule Baraza la Mawaziri wale watamshauri Rais na sio lazima Rais awakubalie walichoshauri. Lakini la pili, masuala yanayojadiliwa na Baraza la Mawaziri pamoja na kwamba ni la ushauri, hayawezi kujadiliwa mahali popote ikiwemo na mahakamani kwa maana ya kwamba huwezi kuhoji maamuzi ya Baraza la Mawaziri mahakamani,” alisema Balozi Silaa na kuongeza:

“Sasa muone taifa linarudi kwenye giza, labda ya karne ya 15 wala sio karne ya 21. Yaani badala ya kupiga hatua mbele, wenzetu wote wanapiga hatua mbele sisi tunapiga hatua 10 nyuma katika mambo ya demokrasia.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!