Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bodi ya Wahandisi watakiwa kuongeza idadi ya Wahandisi washauri
Habari Mchanganyiko

Bodi ya Wahandisi watakiwa kuongeza idadi ya Wahandisi washauri

Spread the love

KARIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Ujenzi), Balozi Mhandisi Aisha Amour amezungumzia umuhimu wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini, ERB kuwawezesha wahandisi washauri wazawa ili kunufaika na kasi ya ukuaji wa uchumi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akifungua, Mkutano wa wataamu wa Wahandisi Washauri jijini Dar es Salaam leo, Balozi Amour amesema ukuaji wa uchumi unaoendelea nchini lazima uendane na ukuaji wa kada ya wahandisi washauri wazawa, na hivyo kuliwezesha Taifa kuwa na wataalamu  wengi watakaofanya kazi  ndani na nje ya nchi.

“Idadi ya kampuni za wahandisi washauri zaidi ya 230 na wahandisi washauri 300 haitoshi, hivyo ibueni mifumo itakayorahisisha wataalam wengi wa kihandisi kusajiliwa kuwa wahandisi washauri na kuweka madaraja mbalimbali ya kada hiyo ili kuongeza ushindani”, amesema Balozi Aisha Amour.

Katibu Mkuu huyo amesema nia ya Serikali ya Awamu ya sita ni kuhakikisha wahandisi wengi zaidi wanatumika katika miradi ya ujenzi na hivyo kunufaika na fedha nyingi zinazolipwa kwa wahandisi washauri  kutoka nje ya nchi.

“Punguzeni masharti ya kusajili wahandisi washauri, hamasisheni wahandisi washauri waliopo kuomba kazi katika miradi inayoendelea, ili fedha nyingi inayoendesha miradi hiyo ibaki nchini”, amesisitiza Balozi, Eng. Aisha Amour.

Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, ERB, Eng. Bernard Kavishe amesema Bodi imejipanga kuhakikisha maazimio yatakayofikiwa kwenye mkutano huo yanafanyiwa kazi kwa haraka ili kuwawezesha waandisi washauri kuongezeka na kumudu ushindani kaitka soko la ndani na nje ya nchi.

“Dunia inabadilika kwa kazi hivyo na sisi wahandisi wa Tanzania tuna wajibu wa kubadilika ili kuendana na mahitaji ya dunia kwa kuhakikisha wahandisi washauri wanakuwepo na wanasajiliwa katika madaraja mbalimbali, ili kuchochea ushindani na kuleta tija kwa Taifa”, Amesema Eng. Kavishe.

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, ERB, Eng. Bernard Kavishe

Mkutano wa mashauriano wa Wahandisi Washauri ni muendelezo wa maelekezo ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ambapo aliitaka ERB kukutana na wadau ili  kujadili na kupatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili Wahandisi Washauri nchini ikiwemo kuongeza idadi na kampuni za wahandisi washauri wazawa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!