Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Biteko akagua mtambo wa Umeme Pangani, atoa maagizo TANESCO
Habari za Siasa

Biteko akagua mtambo wa Umeme Pangani, atoa maagizo TANESCO

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto Biteko amefanya ukaguzi wa mitambo ya umeme inayokarabatiwa katika kituo cha umeme cha New Pangani (MW 68) ambacho kilisimama kuzalisha umeme kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na hitilafu.

Pia amewaagiza wataalam wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kufanya kazi hiyo kwa kasi na umakini ili kukamilisha matengenezo hayo ambayo yapo ukingoni. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katika ziara yake kwenye kituo hicho kilichopo  wilayani Korogwe mkoani Tanga, Dk. Biteko aliambatana na viongozi mbalimbali akiwepo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba.

“Nawapongeza kwa hatua mliyofikia sasa kwenye matengenezo, lakini ni muhimu sana kuongeza kasi na umakini katika kumalizia kazi kwani Watanzania wanatutegemea sisi ili kupata umeme wa uhakika,” amesema Dk.Biteko

Dk. Biteko ameeleza kuwa, matengenezo ya kituo hicho yapo ukingoni na inategemewa kuwa wiki ijayo kitaanza tena kuzalisha umeme na hivyo kuimarisha hali ya upatikanaji umeme hasa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Aidha, ameongeza kuwa, jitihada nyingine zinazofanyika ili kuimarisha hali ya umeme kwenye mikoa hiyo ni kupitia laini ya msongo wa kV 400 itakayotoka Chalinze- Segera hadi Tanga Mjini na laini ya kV 400 kutoka Singida – Manyara- Lemuguru ambayo itaunganishwa na laini ya kutoka Chalinze kwenda Segera hadi Tanga Mjini.

Vilevile, Dk. Biteko amewataka watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa, wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye vituo vya umeme, jambo litakalowawezesha kutambua mapema endapo kuna hitilafu za umeme na kuzifanyia kazi mapema.

Katika hatua nyingine, Dk. Doto Biteko amewasha umeme katika Kijiji cha Ngomeni kata ya Ngomeni wilayani Muheza, Mkoa wa Tanga, na kufanya vijiji vilivyowashiwa umeme wilayani Muheza kufikia 127 kati ya Vijiji 135 sawa na asilimia 95 na katika Vitongoji, Wilaya ya Muheza ina vitongoji 522 na hadi kufikia jana vitongoji 411 vilikuwa vimesambaziwa umeme huku kazi hiyo ikiendelea.

Mara baada ya kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho, Dk. Biteko amesifu umoja uliopo kati ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali katika Mkoa huo, na kueleza kuwa, siri ya mafanikio ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ni viongozi kama hao wanaochapa kazi kwa umoja.

Amesema viongozi wanapogawanyika wanachelewesha maendeleo na kuwaumiza wananchi kwani wananchi wanachohitaji ni huduma bora kama za umeme na maji, hivyo amewaasa viongozi kupendana na kushirikiana, kwani  wanapimwa kwa matokeo ya maendeleo.


Viongozi  walioambatana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, kwa nyakati tofauti wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi na kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali  ya Maendeleo ambapo mpaka sasa Mkoa wa Tanga umepokea Sh 2.6 trilioni kwa ajili ya miradi ya miradi ya maendeleo.

Fedha iliyotengwa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini wilayani Muheza ni Sh 18.96 bilioni ambayo ni kwa ajili ya kusambaza umeme kwenye nyumba, migodi midogo, vituo vya afya, maeneo ya kilimo na pampu na za maji huku mkandarasi akiwa ni kampuni ya Derm Group.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!