Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita
Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the love

Makamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari amesema Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya maji katiam mji mdogo wa Katoro ambao utawanufaishan zaidi ya wakazi 68,000. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Makamu Zainab amesema kuwa lengo la Serikali ni kumaliza tatizo la ukosefu wa maji safi na salama kote nchini.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipotembelea na kukagua mradi wa kuboresha huduma ya maji Mji mdogo wa Katoro-Buseresere wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.1

“Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kusogeza huduma ya maji katika kila nyumba lengo likiwa kumtua mwanamke ndoo kichwani,” amesema Makamu Zainab na kuongeza;

“Wananchi mliopo hapa na wengine wa eneo ili muda si mrefu changamoto ya kufuata maji kwa umbali mrefu itakwisha”.

Ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 92 na unatarajiwa kukamilika mwishoni wa mwezi huu Oktoba mwaka huu 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!