Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa “Bila ya amani, hakuna mtangamano na maendeleo”
Habari za Siasa

“Bila ya amani, hakuna mtangamano na maendeleo”

Spread the love

Nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zimetakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa nchi zao zinakuwa na amani, Umoja na utulivu na kutafuta ufumbuzi wa migogoro kwa  kutumia njia zao wenyewe. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Zambia, Mulambo Haimbe wakati anafungua Mkutano huo uliofanyika jijini Lusaka, Zambia jana tarehe 22 Machi 2024.

Tanzania inatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo baada ya Zambia na inawakilishwa katika Mkutano huo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine unapokea ripoti ya utekelezaji wa vikosi vya kulinda amani katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na mchakato unaoendelea wa kupeleka vikosi vya kulinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Nchi Wanachama zimehimizwa kuimarisha zaidi  mshikamano na kuchangia rasilimali  walizonazo ili kuviangamiza vikundi vya waasi vinavyotishia amani kwenye Kanda ya SADC.  Imeelezwa kuwa bila ya amani na Usalama katika Kanda  hiyo, wananchi wasitarajie kufikiwa kwa mtangamano na maendeleo ya kweli.

Mkutano huo wa Mawaziri ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya SADC utakaofanyika tarehe 23 Machi 2024 ambapo Tanzania itawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!