Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Biashara kuanza kufanyika saa 24 Dar
Habari Mchanganyiko

Biashara kuanza kufanyika saa 24 Dar

Spread the love

UONGOZI wa Mkoa wa Dar es Salaam, unaendelea na vikao vya kuandaa mpango wa wafanyabiashara kutekeleza shughuli zao usiku na mchana (saa 24). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akizungumza na waandishi wa habari, jijini humo.

Chalamila amesema timu za wataalamu kutoka mamlaka mbalimbali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama na  wafanyabiashara zinaendelea kufanya mazungumzo ili kuangalia namna ya kutekeleza mpango huo bila kuleta madhara, huku akiweka wazi kwamba kuna baadhi ya sheria ndogo zitapaswa kurekebishwa ili kutokuwa kikwazo.

“Dar es Salaam ni mji mkubwa, wakati huu tunapoajiandaa kuanza biashara saa 24 kwa kukamilisha soko la Kariakoo, timu zetu zipo kwenye mazungumzo katika vikao vya awali. Taasisi za fedha, vyombo vya ulinzi na usalama na wafanyabiashara na mamlaka nyingine zote tunakamilisha model yetu itakayosaidia kuanzisha biashara kwa muda wa saa 24,” amesema Chalamila.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!