Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya NBC kutoa hatifungani za Bil 30/- kuinua wajasiriamali
Habari Mchanganyiko

Benki ya NBC kutoa hatifungani za Bil 30/- kuinua wajasiriamali

Spread the love

 

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC ) imetangaza utoaji wa hati fungani ya miaka mitano inayofahamika kama NBC Twiga bond, yenye thamani ya Sh. 30 Bilioni, ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati, sekta ndogo ya kilimo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, kiasi cha chini cha ununuzi wa hati fungani hiyo ni Sh 500,000 na inaweza kununuliwa kutoka tawi lolote la Benki ya NBC, au Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) wenye leseni ya udalali.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Hati fungani hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 1 Novemba, 2022, Sabi amesema, “hii ni mara ya kwanza kwa Benki kutoa hati fungani kwa ajili ya umma na ikiwalenga wajasiriamali, wakulima na wafanyabiashara wadogo ambao ndio sehemu kubwa ya ajira za vijana nchini Tanzania.’’

“Wawekezaji katika Hati fungani ya NBC Twiga Bond watapata riba kubwa ya 10% kwa mwaka, inayolipwa nusu mwaka katika kipindi chote cha miaka mitano hadi Novemba 2027. Kiwango cha riba kinacholipwa hakina punguzo la kodi,’’ amesema.

Hati fungani ya Twiga ni ya kwanza kutolewa na Benki ya NBC na inatarajiwa kushughulikia sekta nyingine muhimu za uwezeshaji kiuchumi, changamoto ya ufadhili wa mikopo midogo midogo na ya kati nchini.

Kwa mujibu wa Sabi, ofa hiyo itafunguliwa rasmi tarehe 8 Novemba 2022 na itafungwa tarehe 7 Disemba 2027. Ikishafungwa, hati fungani hiyo ya Twiga itaorodheshwa na kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

“Hii ina maana kwamba mnunuzi wa hati fungani hiyo hiyo ataweza kuuza bondi kwa mnunuzi mwingine katika soko la pili kupitia dalali wa hisa aliyeidhinishwa na kupokea mhusika mkuu kabla ya tarehe ya ukomavu,’’ alifafanua.

Alisema kupitia Hati fungani hiyo benki hiyo inalenga kuongeza zingine zenye thamani ya Sh 300 bilioni ambazo zitatumika katika kufadhili sekta ndogo na za kati, kilimo na sekta nyinginezo muhimu kiuchumi nchini.

“Mapato yatokanayo na Hati fungani ya Twiga yatatuwezesha kukidhi mahitaji ya kifedha kwa ajili ya makundi haya muhimu ambayo yanaajiri watu wengi. Hati fungani ya Twiga NBC iko wazi kwa umma, tukimaanisha zinaweza kununuliwa na watu binafsi, makampuni na taasisi.’’

“Ni matumaini yetu kuwa hatua hii itakuza ufanisi wa uzalishaji, kuongeza ushindani wa soko, na kutetea kanuni bora za utawala na uwajibikaji katika shughuli za biashara. Kama mnavyofahamu, sehemu kubwa ya makampuni ya biashara nchini Tanzania na duniani kote ni ya biashara ndogo na za kati (SMEs), lakini pia yanakabiliwa na mapungufu makubwa ya kifedha ambayo yanazuia ubunifu na ukuaji wa uchumi,’’ amesema Sabi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwakilishi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Brighton Kinemo aliipongeza benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea mikopo nafuu kwa wajasiriamali hususan sekta ya vijana na wajasiriamali wanawake, kwa kuwashirikisha kwenye mipango mbalimbali kama vile akaunti za NBC Shambani na Kua Nasi ili kuongeza ushirikishwaji wa kifedha na kusaidia upanuzi wa mikopo.

“Hati fungani ya Twiga NBC inaonyesha dhamira ya benki NBC kuunga mkono juhudi za serikali kuelekea ushirikishwaji wa kifedha kwa kupanua na kuimarisha Sekta ya Fedha Tanzania kupitia utoaji wa huduma rafiki. Hii ndiyo maana halisi ya ushirikishwaji wa kifedha…hongereni sana” amesema Kinemo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!