Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Exim watambulisha huduma isiyo na mipaka kati ya Tanzania, Comoros
Habari Mchanganyiko

Exim watambulisha huduma isiyo na mipaka kati ya Tanzania, Comoros

Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imetambulisha huduma yake mpya ya kibenki isiyo na mipaka kati ya Tanzania na Comoro inayolenga kutoa miamala ya gharama nafuu kwa wateja na wafanyabiashara kati ya nchi hizo mbili. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akitambulisha huduma hiyo mpya katika soko la Tanzania, Sumit Shekhar, Mkuu wa Idara ya Uwekezaji Kimkakati na Matawi ya Nje wa benki hiyo alisema huduma hiyo inatoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kuweza kufanya miamala ya kifedha kati ya nchi hizo mbili kwa kuwezesha malipo kutoka kwenye akaunti za wateja sambamba na utoaji wa fedha kupitia matawi maalum ya Exim yaliyopo Dar es Salaam, Mtwara na Zanzibar.

Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitambulisha huduma mpya ya kibenki isiyo na mipaka kati ya Tanzania na Comoro inayotolewa na benki hiyo wakati wa hafla fupi ya utambulisho wa bidhaa hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji wa Kimkakati na matawi ya nje wa Benki hiyo, Sumit Shekhar (kushoto), Mkuu wa Bidhaa za Rejareja na Uhakika wa Mapato wa Benki ya Exim, Mtenya Cheya (Kulia) na Meneja Msaidizi wa Biashara na Taasisi za Fedha kutoka benki hiyo, Bruno Tarimo.

“Tunafuraha kuanza huduma hii tukilenga kurahisisha biashara kwa Wacomoro wanaotembelea Tanzania. Kama tunavyojua sote Comoros ni nchi ya visiwa vilivyuopo katika Bahari ya Hindi inayoshiriki mipaka ya baharini na Tanzania kaskazini-magharibi, na tayaru tumeshuhudia kuongezeka kwa maslahi ya biashara kati ya nchi hizo mbili,” alisema Shekhari katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Alitaja baadhi ya bidhaa ambazo zinapelekwa zaidi visiwani Comoros kuwa ni pamoja na  mchele, saruji, samaki, vyakula, sukari, nishati ya mafuta na magari.

“Kwa upande wao wenyewe wanaleta Tanzania zaidi karafuu, vanila, na vyombo vya usafiri wa majini. Tanzania yenye idadi kubwa ya makampuni ya viwanda nchini na miundombinu mikubwa ya bandari inatoa ushirikiano mkubwa wa kibiashara kati ya nchi zote mbili. Hivyo bidhaa hii inalenga kurahisisha hilo,” aliongeza Shekhar.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Andrew Lyimo alisema hatua hiyo ni mwendelzo wa mkakati wa benki hiyo wa kuongeza ufanisi wa huduma zake za kibenki za kielektroniki ili kuwapa wateja huduma bora zaidi pamoja na kujitanua zaidi katika ukanda wa Afrika.

“Exim ni kati ya benki tano bora nchini Tanzania na benki kubwa zaidi katika visiwa vya Comoros na ni taasisi pekee ya kifedha kuwa na uwepo wake katika nchi zote mbili. Ujio wa huduma hii pamoja na faida za kibiashara na zile za kijamii pia utasaidia kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili na pia kutengeneza fursa kwa wafanyabiashara na wazalishaji katika nchi zote mbili,’’ alisema Lyimo

Kwa mujibu wa Lyimo, kupitia bidhaa hiyo, raia wa Comoro anayetembelea Tanzania kwa sababu za biashara, matibabu au madhumuni yoyote anaweza kutoa fedha au kufanya malipo ya huduma hizo wakati wowote akiwa hapa nchini bila kuathiriwa na sababu za kimipaka baina ya mataifa haya mawili.

“Wanachohitaji wateja ni kutembelea matawi yetu mahususi kwa ajili ya huduma hii yaliyopo Dar es Salaam, Mtwara na Zanzibar hivyo kuwarahisishia kufanya biashara na kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari na usumbufu wa kufanya biashara kwa fedha taslimu,” alitaja.

Matumizi ya huduma hiyo yanatajwa kuwa yatawanufaisha wateja wa benki hiyo kwa faida kadhaa zikiwemo; kusafiri bila pesa taslimu pamoja na urahisi, uharaka, na njia ya kuaminika ya kutoa pesa nje ya nchi.

“Zaidi kupitia huduma hii wateja wetu wanaweza kufanya malipo mbalimbali kutoka kwenye akaunti zao wakiwa nje ya nchi, kujikinga na hatari ya wizi na upotevu wa fedha na pia inawawezesha kutumia fedha zao kulingana na mahitaji yao,’’ alitaja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!