Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Babu Owino: Vijana msibaki nyuma
Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Babu Owino
Spread the love

Mbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu ‘Babu Owino’ amewaasa vijana kuwa chachu ya mageuzi ya kisiasa ili kuwaletea mabadiliko wananchi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea)

Babu Owino ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ODM cha Kenya amesema hayo leo tarehe 29 Februari 2024, katika Mkutano Mkuu wa Ngome ya Vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania.

Babu Owino amesema vijana kuwa mstari wa nyuma kwenye mapambano ya kusaka madaraka kunawakosesha haki ya uwakilisha na sauti yao kutokuwepo kwenye vyombo vya uamuzi.

“Mwalimu Nyerere, Nelson Mandela na Jomo Kenyata walipambania uhuru na ukombozi wakiwa vijana”

Amesema vijana ni lazima wahakikishe wanaingia kwenye mapambano ya madaraka.

“Kijana usipokuwa kwenye meza ili ule basi utakuwa kwenye menu uliwe hakika usipokuwepo kwenye mapambano hutakuwepo kwenye meza.

Ngome ya Vijana ya chama hicho inafanya uchaguzi wa kusaka Mwenyekiti wa chama hicho, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu kupitia Ngome hiyo.

Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti inagombewa na Abdul Nondo anayetetea kiti chake, Julias Masabo, Ndolezi Petro na Ruqaiya Nassir.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!