Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro
Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Maparachichi
Spread the love

IMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia katika mkoa wa Morogoro limetajwa kuwa miongoni wa zao la kimkakati ambalo linatarajiwa kuongeza  kipato cha mkulima sambamba na  ajira kwa wakazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro… (endelea).

Akizungumza na mwandishi wa habari mkoani hapa, Meneja wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda ya Juu Kusini (SAGCOT) Kongani ya Kilombero, John Banga amesema mbali kuupaisha mkoa, kilimo cha karafuu ambacho kinalimwa pamoja parachichi ni mazao yanayowavutia wakulima wengi.

“Wakulima wa karafuu mkoani hapa wamekuwa wakilima kwa ustadi mkubwa sambamba na kupewa mafunzo na safari za mafunzo Zanzibar ambako ni chimbuko la zao hili la karafuu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Banga.

Meneja huyo amesema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana SAGCOT imeshawapeleka wakulima Zanzibar kujifunza namna bora ya kuendeleza kilimo cha Karafuu hapa nchini.

“Serikali imekuwa ikitoa msaada wa taarifa za masoko, pembejeo, upatikanaji wa kifedha kwa wakulima na utoaji wa mafunzo kupitia safari za visiwani Zanzibar ili kujifunza kwa wakulima wenzao  na kuongeza  tija katika uzalishaji,” amesema.

Kwa mujibu wa Banga, Mkoa wa Morogoro hususani  katika wilaya  zake za  Gairo, Mvomero na Kilombero zimekuwa  na hali hewa nzuri pamoja na  ardhi nzuri inayofaa kwa  kilimo cha karafuu.

Amesema SAGCOT kupitia wabia wake mbalimbali wakiwemo IUCN, AWF, WWF na wadau wengine wa maendeleo wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na wakulima katika kuboresha kilimo cha karafuu.

“Mwaka 2023, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na SAGCOT waliwezesha ziara ya wakulima zaidi ya 50 na wataalam wa mikoa ya Morogoro na Tanga kujifunza  Zanzibar namna ya kuongeza thamani kwenye mazao ya viungo ikiwemo karafuu,” amesema.

Amesema kufuatia  ziara hiyo, wadau walielekeza nguvu kwenye uzalishaji wa miche bora ya karafuu hadi mwezi huu  (Februari 2024), zaidi ya miche laki tatu na nusu imezalishwa katika Wilaya ya Morogoro pekee ambapo miche hiyo inatarajiwa kupandwa kwenye mashamba ya wakulima wadogo zaidi ya elfu tano.

Banga amesema Wilaya ya Gairo pekee kuna zaidi ya wakulima 500 ambao wamehamasika kufanya kilimo cha karafuu na wakulima zaidi ya 40 wameshapewa mafunzo maalumu ya kilimo cha kisasa cha parachichi kutoka mkoani Njombe.

“ Tunategemea kupitia zao la karafuu mapinduzi makubwa ya kiuchumi na matokeo chanya katika kukuza pato la mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla wake ,” amesema Banga. nakuongeza kuwa zao hilo jipya linaratibiwa na SAGCOT  kupitia Kongani yake Kilombero.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!