Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu aliburuza kanisa la Kakobe mahakamani
Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu aliburuza kanisa la Kakobe mahakamani

Askofu Zakaria Kakobe
Spread the love

BARAZA la Usuluhishi wa Migogoro ya Ardhi Kata ya Bahi mkoani Dodoma limeahirisha kesi ya malalamiko ya ardhi iliyofunguliwa na Askofu mkuu wa Kanisa wa Kanisa la Glory to God Ministry (GGM), Dk. Benson Rutta dhidi ya Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Kanda ya Kati, Neema Mduma baada ya mlalamikiwa kushindwa kufika mbele ya baraza. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kesi hiyo iliyosikilishwa leo Alhamis na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Wilaya ya Bahi, Maneno Dikson imeahirisha hadi tarehe 14 Desemba 2023.

Mwenyekiti na baraza lake wamelazimika kuahirisha kesi hiyo kutokana na mlalamikiwa Askofu Neema Mduma kushindwa kufika kwenye kesi hiyo.

Askofu Dk. Benson Rutta

Askofu Dk. Rutta amemfungulia shauri Askofu Neema Mduma wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship linaloongozwa na Askofu Zakaria Kakobe, kwa madai ya kumpora jengo lake la kanisa lililopo wilaya ya Bahi.

Askofu Mduma ambaye anaongoza kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lenye makao makuu yake Maili mbili Jijini Dodoma, anadaiwa kung’ang’ania jengo hilo kwa madai kuwa ni mali ya kanisa la Full Gospel Bible Fellowship jambo ambalo linapingwa na Askofu.Dk Rutta.

Hata hivyo, katika shauri hilo ambalo lilikuwa lisikilizwe kwa mara ya pili lakini baraza lilikataa kuendelea na usuluhisho baada ya Askofu Neema Mduma kushindwa kufika huku aliydaiwa kuwa mwakilishi wake akidaiwa kutokuwa na utambulisho wowote.

Awali kabla ya Askofu Dk. Rutta kuanzisha huduma yake alikuwa Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship wilayani Kondoa na baada ya kujiengua katika huduma ya Askofu Zacharia Kakobe, Dk.Rutta alidai kuporwa mali zake zote ambazo alikuwa akizimiliki.

Kutokana na hali hiyo Askofu Dk. Rutta alisema kutokana na uonevu alioupata atahakikisha anafuata sheria kwa nia ya kupata haki yake ambayo amedhulumiwa na kanisa la Full Gospel Bible Fellowship.

Kwa upande wake aliyekuwa mwakilishi wa Askofu Neema Mduma wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Jimbo la Dodoma, George Mtega ambaye amekataliwa na baraza ameahidi kuwa tarehe 14 Desemba 2023 atapeleka vielelezo vyote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!