Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Anne Makinda kutunuku wahitimu 291 HKMU
ElimuHabari

Anne Makinda kutunuku wahitimu 291 HKMU

Spread the love
SPIKA Mstaafu ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki (HKMU), Anne Makinda anatarajiwa kuwatunuku wahitimu 291 wa masomo mbalimbali kwenye mahafali ya 20 ya Chuo hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Yohana Mashalla, amesema leo kuwa mahafali hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 3 Desemba 2022 yatatanguliwa na Kusanyiko la Wahitimu (Convocation) siku ya Ijumaa tarehe 2 Desemba 2022 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa Marekani nchini.

Alisema kauli mbiu ya kusanyiko hilo la wahitimu mwaka huu ni “kukuza ubunifu ili kuimarisha mifumo ya utoaji wa afya”  na kuongeza kuwa kwenye tukio hilo wanafunzi waliofanya vizuri (best students) katika mitihani yao watapewa zawadi mbalimbali.

Kuhusu Mahafali alisema, yatahudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Afya na Elimu Kairuki (KHEN), Kokushubira Kairuki na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha (HKMU) Bwana John Ulanga, viongozi wa Serikali katika ngazi mbalimbali, wadau wa mendeleo na wageni waalikwa.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Profesa Yohana Mashalla

Alisema kwenye mahafali hayo kutakuwa na jumla ya wahitimu 291, kati yao wanawake ni 170 na wanaume ni 121.

Aliongeza kuwa wahitimu 54 watatunukiwa Stashahada ya Uuguzi, 10 Stashahada ya Ustawi wa Jamii, 38 Shahada ya Uuguzi. Wahitimu 177 watatunukiwa Shahada ya Udaktari wa Binadamu kati yao wanawake ni 97 na wanaume ni 80.

Profesa Mashalla aliongeza kusema kwenye mahafali hayo pia jumla ya wahitimu 12 watatunukiwa shahada za Uzamili, kati yao 10 watatunukiwa Shahada ya Uzamili ya Tiba na Afya ya Watoto (MMED, Peadiatrics and Child Health).

3.Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Elimu ya Afya Kairuki (KHEN), Kokushubira Kairuki

Alisema mwanaume mmoja atatunukiwa Shahada ya Uzamili ya Upasuaji (MMED, surgery) na mwanamke mmoja atatunukiwa Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Afya ya Jamii (MSc, Public Health).

“Nawapongeza wahadhiri, maprofesa pamoja na watumishi wote wa HKMU kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya kuwalea na kuwafundisha wahitumu wote wanaotarajiwa kutunukiwa vyeti, stashahada na shahada siku ya Jumamosi,” alisema Profesa Mashalla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

error: Content is protected !!