CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema mabadiliko ya sheria ya vyombo vya habari yataakisi maendeleo ya tasnia hiyo pamoja na maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dk. Rose Reuben ametoa kauli hiyo leo tarehe 29 Novemba, 2022 wakati akichangia mjadala wa mabadiliko ya sheria ya vyombo vya habari ulioendeshwa na Jukwaa la Wahariri nchini TEF.
Amesema kuwa suala la mabadiliko ya sheria ambalo limewashirikisha wadau wote wa habari ni jambo jema.
Ametoa wito kwa wadau wote kutoa mawazo chanya yatakayoleta mabadiliko.
“Pia uwajibikaji wetu kama wadau tunapaswa kutoa mawazo yetu lakini kufika pahali ambapo tunaweza kukubaliana ili kufanya mchakato wa sheria uende haraka iwezekanavyo,” amesema.
Dk. Rose alisema mabadiliko hayo yatawabadilisha waandishi kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma lakini pia nchi itapata maendeleo kutokana na kuendelea kwa tasnia hiyo.
Leave a comment