Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya ‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni
Afya

‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni

Spread the love

Wananachi wa  Tarafa ya Mkuyuni, Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro, wameepukana na adha ya kukodi magari ya kubebea wagonjwa kwa gharama kubwa kutoka kwa watu binafsi baada ya serikali kuwapatia gari maalumu la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Mkuyuni kinachohudumia wananchi wote wa tarafa ya Mkuyuni. Anaripoti Victor Makinda, Morogoro…(endelea).

Wakizungumza kwa furaha kwenye halfa ya kukadhiwa kwa gari hilo la wagonjwa jana Jumapili kwenye kituo hicho cha afya,  wananchi hao walimpongeza Mbunge wa Morogoro Kusini Mshariki, Hamis Taletele na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaptia gari hilo la wagonjwa.

Walisema gari hilo litaleta ukombozi mkubwa kwao kwa kuwa walikuwa wakilazimika kukodi magari kwa watu binafsi kwa fedha nyingi pindi wagonjwa wao wanapopata rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyo umbali wa Kilometa 35.  

“Hapa kwenye kituo chetu cha afya tunapata huduma nzuri za matibabu na hata operesheni za uzazi zinafanyika,  lakini  tunapopewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa, kwa kweli tulikuwa tunateseka sana hasa sisi akina mama na watoto,” alisema Zainabu.

Akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi gari hilo la wagonjwa, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Msahariki, Hamis Taletele, (CCM) alisema kuwa gari hilo ni miongoni mwa ahadi zake alizozitoa kwa wananchi wa Tarafa ya Mkuyuni kuwa angeliwapatia gari la wagonjwa kwenye kituo hicho cha afya ili liweze kuwa msaada kwao pindi wanapopata rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi.

“ Niliwaahidi kuwa kabla sijamaliza kipindi changu cha miaka mitano ya ubunge, nitahakikisha wananchi wa Mkuyuni mnapata gari ya wagonjwa kwenye kituo chenu cha afya.

“Sasa ninatekeleza ahadi yangu, nimepambana serikali yenu ya CCM imewapatia gari hilo,” alisema Taletale.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro, Lukas Lemomo aliutaka uongozi wa kituo cha Afya Mkuyuni, kulitunza gari hilo sambamba na kulitumia kwa malengo mahususi. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!