Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT yamkaalia kooni Bashe, yamtwisha zigo la wakulima
Habari za Siasa

ACT yamkaalia kooni Bashe, yamtwisha zigo la wakulima

Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema atawasilisha kwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, changamoto zinazowakabili wakulima wa Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songea … (endelea).

Masoud ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alitoa msimamo huo jana tarehe 14 Januari 2024, wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Ruvuma.

Mwanasiasa huyo alitoa msimamo huo baada ya kupokea changamoto nyingi za wakulima wa Songea hasa zinazohusu upatikanaji, usambazaji wa pembajeo na ununuzi wa mazao na kwamba atazifikisha changamoto hizo kwa viongozi wenye dhamana Serikalini ikiwemo Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

“Nimeelezwa hapa kuwa licha ya jitihada ambazo Serikali imezichukua kwenye upatikanaji na usambazaji wa pembejeo, bado hali si nzuri kwa wakulima wa Ruvuma hasa kwenye eneo la upatikaji wa mbolea. Nimeelezwa, katika msimu uliopita wa kilimo, mbolea badala ya kugaiwa vijijini waliko wakulima, inagaiwa mjini. Nimeelezwa pia mbolea imekuwa haipatikani kwa wakati,” alisema Masoud.

Masoud alisema “Nimeelezwa pia licha ya ahadi ya Serikali kununua mahindi tani 500,000 kupitia hifadhi ya taifa ya chakula, bado wakulima hawakuweza kulipwa bei nzuri na kwa wakati. Sisi ACT Wazalendo, hoja yetu ni kuwa Serikali inapaswa kuimarisha bajeti na uwezo wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), ili kuwanusuru wakulima wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla.”

Maoud alisema Ruvuma ambao ni mkubwa kuliko nchi ya Rwanda, hauna sababu ya kuendelea kuwa masikini kwa sababu ya kubarikiwa rasilimali nyingi, ikiwemo ardhi yenye rutuba na vyanzo vya maji.

Masoud anaendelea na ziara yake ya ujenzi wa Chama katika mikoa ya Ruvuma, Mkoa wa Kichama Selous, Lindi, Mtwar, Pwani na Dar es salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

error: Content is protected !!