August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo waibua hoja sita bodi ya mikopo

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu

Spread the love

 

NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT Wazalendo nchini Tanzania imebuka na hoja sita dhidi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), hali inayosababisha baadhi changamoto za wanafunzi kutoisha, ikiwemo ufinyu wa bajeti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumapili tarehe 5 Juni 2022 na Mwenyekiti wa Ngome hiyo, Abdul Nondo, wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi kuu za chama hicho, Kijitonyama wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Nondo alisema kwa muda mrefu kumekuwa na ufinyu wa Bajeti katika utoaji wa mikopo elimu ya juu ukilinganisha na idadi ya wanafunzi walioomba na wenye sifa za kupata mkopo.

“Hata katika taarifa ya CAG ya 2020/2021 ameelezea juu ya wenye sifa kukosa mikopo sababu ya mifumo na uhaba wa fedha na ajeti. Changamoto hii imejitokeza tena 2021/2022 mbali na kwamba Bajeti ya mkopo elimu ya juu iliongezwa mwaka 2021 kufikia Sh.bilioni 570,” alisema.

Alisema kati ya wanafunzi 160,000 wanafunzi wa mwaka wa kwanza ni 62,000 na wanaoendelea ni 98,000 tofauti na mwaka juzi 2020 ambapo Serikali ilitoa Sh.bilion 464.

Nondo alisema kutokana na kadhia hiyo wanapendekeza Serikali iongeze fedha ya kutosha katika Bajeti ya bodi ya mikopo katika mwaka wa fedha unaoingia, tathimini inaonesha zaidi ya wanafunzi laki moja wanatarajia kujiunga na chuo kikuu.
Mwenyekiti huyo ameitaka bodi ya mikopo igawe mikopo kwa wanafunzi kwa lengo la kusaidia kumudu gharama za masomo kulingana na mgawanyo unaotakiwa, bodi hiyo.

Nondo alisema hoja ya pili ambayo wanataka ipatiwe ufumbuzi kwa haharaka ni kuhusu njia iliyotumika kufuta tozo na ada ya kutunza thamani ya mkopo asilimia 6 mbapo ngome ya vijana baada ya kufanya tafiti ya kisheria kumeonekana kuna changamoto na ukakasi katika meneno ya kisheria yaliyotumika.

“Maneno yaliyotumika tozo hizi hazijafutwa baada ya tamko la Rais na waziri kufuta tozo hizi, Bunge lilifanya marekebisho ya sheria ya Bodi ya Mikopo Sura.178 kifungu cha 7 (2) kupitia sheria ya fedha Na. 3 ya mwaka 2021 kifungu cha 18, marekebisho haya yaliizuia bodi kutoza tozo/ada hizi bila idhini ya waziri wa elimu baada ya kushauriana na waziri wa fedha na mipango.

Kwa tafsiri hii ya kisheria ni kwamba tozo hazijafutwa isipokuwa bodi ya mikopo imezuiwa kutoza bila idhini ya waziri wa elimu hivyo siku yeyote Serikali kupitia waziri wa elimu wanaweza kutoa idhini bodi ya mikopo iaendelee kutoza tozo hizi,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema wanapendekeza Serikali kupitia wizara ya elimu ipeleke muswada bungeni wa marekebisho ya sheria ya bodi ya mikopo, kifungu kitamke waziwazi ndani ya sheria bodi ya mikopo haina mamlaka ya kutoza tozo ya adhabu, tozo ya kutunza thamani ya mkopo au tozo yeyote kwa mnufaika wa mkopo.

Nondo alisema hoja yao ya tatu ni kitendo cha HESLB kutoza tozo ya utawala asilimia moja mara moja kwa kila mnufaika kugharamia shughuli za kiutalawa za bodi.

“Hili ni jambo ambalo bodi ya mikopo wanapaswa kutolea maelezo, kwa sababu kuu mbili. Mosi bodi hii ni ni taasisi tendaji ya Serikali, inapokea fedha ya kujiendesha kutoka baada ya kuidhinishwa na bunge kwenda bodi ya mikopo kupitia wizara ya elimu kwa ajili ya gharama za kiutendaji na kiutawala.

Mbili, Juni 2021 Bunge lilifanya marekebisho ya sheria ya Bodi ya Mikopo Sura.178 kifungu cha 7 (2) kupitia sheria ya fedha Na. 3 ya mwaka 2021 kifungu cha 18, marekebisho haya yaliizuia bodi ya mikopo kutoza tozo yeyote bila idhini ya waziri wa elimu baada ya kushauriana na waziri wa fedha na mipango,” alisema.

Mwenyekiti huyo aliitaka bodi hiyo iheshimu sheria na kuache kutoza tozo kwamadai kuwa naibia wanufaika na kuitaka wizara ya elimu iingilie kati.

Nondo alisema hoja yao ya nne ni kuiomba Serikali kuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wanaopata mikopo kutokana na gharama za maisha kupanda.

“Kuanzia mwaka 2015 hadi sasa wanafunzi wanapokea Sh.8,500, hivyo tunapendekeza Serikali iongeze kiasi cha fedha ya kujikimu hadi Sh. 9500 au zaidi kwa siku kutokana na kupanda kwa gharama za maisha,” alisema.

Alisema ngome hiyo inapingana na hotuba ya waziri wa elimu Profesa Adolf Mkenda wakati akiwasilisha bajeti bungeni ambapo alisema Serikali imekubaliana na Benki ya NMB kutoa mikopo yenye riba kwa wanafunzi.

“Kwetu sisi Ngome ya vijana ACT Wazalendo na chama chetu tumeona huu sio msaada bali ni njia ya serikali kukwepa majukumu yake ya kugharamia elimu,” aliongeza.

Mwenyekiti huyo alisema hoja ya tano mwisho ni kuhusu mifumo ya bodi hiyo kudaiwa kuingeza madeni kwa wadaiwa, hivyo wana wajibu wa kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo.

Nondo alisema wanaitaka bodi hiyo ifanye uhakiki ili kutambua wadaiwa wote ambao wameongezewa deni kwa sababu ya mifumo yao ili kuondoa deni lililoongezeka.

Alisema bodi ya mikopo imalize mchakato wa uunganishaji mfumo wa mkopo na mfumo wa mishahara wa serikali ili kuondoa changamoto hiyo.

Nondo alisema hoja ya mwisho wanaitaka Serikali ipunguze makato kutoka asilimia 15 hadi chini ya asiklimia 8 ili kuwezesha wanufaika kufanya shughuli za maendeleo.

error: Content is protected !!