July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwaikali avuliwa hadhi ya Uaskofu

Spread the love

 

KANISA la Kiinjili la Kulutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde imetangaza kumwondolea wakfu wa Uaskofu, Dk. Edward Mwaikali aliyekuwa askofu wa Dayosisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Aidha, imeviondolea wakfu vifaa vya Kiaskofu alivyokuwa anatumia pete, msalaba na fimbo ambavyo alikabidhiwa tarehe 18 Januari 2018 alipowekwa wakfu kuiongoza Dayosisi ya Konde.

Uamuzi huo umefanyika leo Jumapili tarehe 5 Juni 2022 wakati wa Ibada ya kumweka wakfu mrithi wake, Dk. Geofrey Mwakihaba.

Wamefikia hatua hiyo baada ya Dk. Mwaikali kugoma kuvirejesha ili vitumike kwa mrithi wake kwa mujibu wa taratibu za kanisa hilo.

Dk. Mwaikali aliondolewa madarakani tarehe 22 Machi 2022 na Mkutano Mkuu Maalum wa KKKT Dayosisi hiyo kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuiongoza vyema.

Vitu vingine ambavyo amegoma kuvirejesha ni kiti cha uaskofu na mavazi ambavyo navyo vimeondolewa wakfu.

error: Content is protected !!