Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo: Hatutabakisha jimbo Pemba
Habari za Siasa

ACT Wazalendo: Hatutabakisha jimbo Pemba

Spread the love

WAKATI joto la Uchaguzi mkuu likizidi kupanda, Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kutokana na mikakati ya ushindi iliyowekwa, wana uhakika wa kushinda majimbo yote kisiwani Pemba katika uchaguzi huo. Anaripoti Mwandishi wetu…(endelea).

Hayo yamebainishwa jana na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ado Shaibu wakati akihutubia wananchi kwenye ziara yake kisiwa hapo.

Ado amesema chama hicho kinatembea kifua mbele kwa kuwa tayari kimesajili wanachama zaidi ya nusu ya wapigakura wote wa majimbo yote Pemba.

“Hii ni ishara kuwa majimbo haya yote 18 ni ya ACT Wazalendo. 2025 tutahakikisha tunayarejesha majimbo yote mikononi mwetu,” amesema Ado.

Amesema hamasa ya wanachama wao inaonesha kuwa watayakomb majimbo yote kutoka kwenye mikono ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Hamasa mnayoionesha hapa Pemba kulipia ada za uanachama katika siku za karibuni ni ishara kuwa tukiongeza juhudi, chama hiki kinaweza kuendeshwa na wanachama kwa asilimia 100,” alisema.

Ado alisema kuwa kipaumbele cha Chama hicho ni kupigania mamlaka kamili ya Zanzibar.

“Wazanzibar wanajua wanachokitaka. Hakijawahi kubadilika tangu enzi za chama kimoja hadi enzi za vyama vingi. Wazanzibar wanataka mamlaka kamili. Wazanzibar wanataka Muungano wa haki, usawa na heshima baina ya pande mbili za muungano” amesema Ado.

Mengine yaliyoadhimiwa na chama hicho ni pamoja chama kuendeshwa na wanachama kupitia mfumo wa ACT- Kiganjani na ada za wanachama, kufanya uchaguzi ndani ya chama na mageuzi ya kisiasi visiwani humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!