Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT kumsaka mrithi wa Maalim Seif ACT Oktoba 31
Habari za Siasa

ACT kumsaka mrithi wa Maalim Seif ACT Oktoba 31

Janeth Rite, Naibu katibu mwenezi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

 

HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT Wazalendo inatarajiwa kuketi tarehe 31 Oktoba mwaka huu huku jambo kubwa likitarajiwa kumsaka mrithi nafasi ya Uenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo ambayo ipo wazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa baada ya aliyekuwa ameshikilia nafasi hiyo Hayati Maalim Seif Sharif Hamad kufariki dunia Februari 17 mwaka huu. Anaripoti Mwandishi wetu… ( endelea).

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 27 Oktoba, 2021, Dar es Salaam Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa chama hicho, Janeth Rite amesema Halmashauri Kuu itakayoketi tarehe 31 Oktoba, 2021 itatangaza mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti Taifa.

Amesema mbali na hilo, Halmashauri Kuu ya Chama hicho itaketi kwenye kikao chake cha kawaida katika Ukumbi wa Hoteli ya Landmark Dar es salaam na kitatanguliwa na Kikao cha Kamati Kuu itakayoketi tarehe 30 Oktoba 2021 katika Ukumbi huohuo.

“Halmashauri Kuu ya Chama Taifa ni kikao cha pili kwa ukubwa baada ya Mkutano Mkuu Taifa. Halmashauri Kuu ya Chama inajumuisha wajumbe wote wa Kamati Kuu, Wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Kuchaguliwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Kuteuliwa.

“Wengine ni Makatibu na Wenyeviti wa Mikoa, Wawakilishi wa Makundi Mbalimbali kama vile Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Madiwani, Watu Wenye Ulemavu pamoja na Ngome za Chama za Vijana na Wazee na Wanawake.

“Hii ni Halmashauri Kuu ya kwanza kuketi baada ya Uchaguzi Mkuu 2020 ambao uligubikwa na udanganyifu, hila na hujuma kubwa.

“Hivyo basi, pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Chama Taifa itapokea Taarifa ya Uchaguzi Mkuu 2020 na kuijadili” amesema Rithe.

Aidha, Rithe ameongeza Halmashauri Kuu itapokea pia Taarifa ya Kamati Kuu ya Hali ya Chama katika kipindi cha mwaka mmoja kwa maana ya tangu Oktoba 2020 hadi Oktoba 2021.

Amesema kwa kuwa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa iko wazi, Halmashauri Kuu hii itatangaza mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa.

“Taarifa zaidi ya mchakato mzima wa uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo, itatolewa baada ya kikao cha Halmashauri Kuu.

“Halmashauri Kuu ya Chama Taifa itapokea pia Taarifa ya Hali ya Kisiasa ndani ya Chama, Nchi na Kimataifa, kuijadili na kutoa mwelekeo wetu wa kisiasa wa ndani na nje ya nchi” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!