Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya NBC yaja na kadi mpya, inafanya miamala hadi ya mil 40
Habari Mchanganyiko

Benki ya NBC yaja na kadi mpya, inafanya miamala hadi ya mil 40

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC Elibariki Masuke (wanne kushoto) pamoja na mteja mmoja wa wateja wa benki hiyo, Scholastica Ponela (wa tatu kulia) wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa kadi mpya za benki hiyo zinazofahamika kama ‘NBC Visa Debit Card’
Spread the love

 

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kadi mpya ‘NBC Visa Debit Card’ yenye kuwawezesha wateja binafsi kufanya miamala inayofikia hadi Sh milioni 40 kwa mara moja ilihali wateja wa kawaida wakifanya miamala inayofikia milioni 10 kwa mara moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …  (endelea).

Akizindua kadi hiyo mpya ya kidijitali ikiwa na muonekano wa wima, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC, Elibariki Masuke alisema kadi hiyo inaiwezesha NBC kuunganisha mifumo yake mbalimbali ya malipo kwa njia tofauti mbalimbali.

“Tunazindua kadi yetu yenye nembo maarufu ya Twiga inayotambulisha Benki ya NBC. Kadi hii ina teknolojia ya NFC yaani tap and go.

“Kwa kutumia teknolojia iliyopo kwenye kadi hii, itatupatia uwezo wa kufanya malipo katika sehemu ambazo benki inatoa huduma kama vile viwanja vya michezo, usafiri wa umma ambao ni treni, magari ya mwendokasi na sehemu nyingine.

Akiizungumzia zaidi kadi hiyo Masuke alisema ni salama kwa matumizi kwani imethibitishwa na VISA International hatua ambayo inaiwezeshwa kufanikisha miamala ya ndani na nje ya nchi.

Pia kadi hiyo ina uwezo wa kudumu kwa muda wa miaka mitano bila kuharibika.

Maofisa wa benki ya NBC wakionesha muonekano wa moja ya kadi mpya za Benki hiyo zenye muonekano wa wima wakati wa hafla hiyo.

 

Alisema kadi hiyo inatolewa kwa wateja wapya pindi wanapofungua akaunti na wale wenye akaunti ndani ya NBC wanaweza kwenda kwenye matawi ya benki hiyo na kupatiwa kadi hizo.

“Ni kadi bora kwani inapopita kwenye mashine za ATM haina mkwamo-mkwamo,” alisema.

Aidha, Mkuu wa Kitengo cha huduma za Benki Kidijitali –NBC, Deogratius Mosha alisema uzinduzi wa kadi hiyo unatokana na matunda ya ubunifu wa kazi zinazofanywa na benki hiyo.

“Kwa miaka 10 Benki ya NBC imekuwa ikiwekeza katika mifumo ya kiteknolojia na rasilimali watu ili kuhakikisha benki inakuwa namba moja katika utoaji wa huduma za benki kidijitali hapa nchini.

Maofisa waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC Elibariki Masuke (katikati) wakifuatilia uzinduzi huo

“Tumejikita katika uundaji wa mifumo mbadala, kuwezesha wateja wetu kupata huduma za benki popote walipo bila kufika katika matawi ya benki,” alisema.

Alisema mifumo hiyo inajumuisha huduma zinazopatikana katika mashine za ATM, ambazo ni utoaji wa huduma za kibenki kwa njia ya simu, miamala ya kibenki na huduma nyingine.

“Pia kuna dawati maalumu la ubunifu ambalo linasimamia ubunifu wa bidhaa na mifumo inayolenga kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma za kibenki pamoja na kuboresha huduma kwa wateja waliopo hapa nchini na wale waliopo nje ya nchi,” alisema.

Aidha, alisema Benki hiyo itaendelea kuwekeza katika ubunifu wenye tija na kutoa huduma ambazo zinakidhi matakwa kwa wateja wa benki hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!