Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba
Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the love

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro kuhusu ukaguzi wa pasipoti kwa mashabiki watakaovaa jezi za timu za Mamemodi Sundown na Al Ahly kuwa ulikuwa ni utani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Ndumbaro alisema mashabiki hao ambao wataingia katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kushangilia kwenye michezo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayohusisha Simba na Yanga kati ya timu hizo za Afrika Kusini na Misri, watatakiwa kuonesha pasipoti za uraia wa nchi hizo.

Matinyi ametoa ufafanuzi huo leo Jumapili wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kutoja vyombo mbalimbali leo Jumapili kuhudu miaka miatu ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema “Katika lugha za michezo utani ni kitu cha kawaida, mnapozungumza 80% ni utani na 20 ndio ukweli, mkizungumza habari za Simba na Yanga ukang’ang’ana kitu kama kilivyoandikwa utafika hatua utawachosha watu.

“Hizo ni timu ambazo zinapenda utani, zinapokea ujumbe katika lugha rahisi, si kweli kuwa Waziri alimaanisha kutakuwa na ukaguzi wa Passport, anayehusika na ukaguzi halali ni Idara ya Uhamiaji ambayo hakuitaja alipozungumza,” amesema.

Matinyi ameongeza kuwa “Watu wamekomaa na utani hadi Mamelodi wamesikia, wameingia uoga hadi TFF wameamua kuandika barua kuwaeleza suala hilo halipo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

error: Content is protected !!