Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa ‘Wachawi’ 50 wafariki baada ya kumeza dawa mitishamba
Kimataifa

‘Wachawi’ 50 wafariki baada ya kumeza dawa mitishamba

Spread the love

Watu zaidi ya 50 wanaoshutumiwa kwa ‘uchawi’ wamefariki dunia nchini Angola baada ya kulazimishwa kunywa mchanganyiko wa mitishamba ili kubaini kama wanafanya vitendo vinavyochukuliwa kuwa vya kichawi au lah! Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Waangola wengi hukimbilia kwa ‘wachawi’ waliopewa mamlaka ya juu zaidi kulingana na baadhi ya imani, kutatua mzozo au kabla ya kufanya uamuzi. Vitendo hivi vinapingwa hasa na Kanisa katika koloni hili la zamani la Ureno lenye wakatoliki wengi.

Ofisa mteule wa manispaa ya Camacupa, Luzia Filemone alieleza redio ya taifa hilo kuhusu vifo hivyo na kudai kuwa vifo vimeongezeka kwa kasi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

“Zaidi ya waathiriwa 50 walilazimishwa kunywa maji haya ya ajabu ambayo, kwa mujibu wa washauri wa jadi, yanathibitisha kwamba mtu huyo anafanya uchawi au lah,” alisema.

Aidha, Mkuu wa Polisi kayika eneo hilo, António Samba alisema; “Idadi ya vifo vilivyohusishwa na unywaji wa kioevu hiki iliongezeka kutoka 30 hadi 50.”

Hakuna sheria nchini Angola inayoadhibu rasmi ‘uchawi’, lakini kiutendaji, ‘wazee wa busara’ wanaochukuwa nafasi ya washauri ndani ya baadhi ya jamii wanashauriwa ili kubaini kama mtu ni mchawi.

Mchakato huo unahusisha kuwafanya wale wanaoitwa wachawi kumeza kinywaji cha mitishamba kiitwacho “mbulungo.”

Kwa mujibu wa baadhi ya imani, mtu akifa baada ya kunywa maji hayo, basi inathibitishwa kwamba alikuwa akifanya uchawi.

“Ni tabia iliyoenea sana kunywa sumu inayodhaniwa kuwa kwa sababu ya imani ya uchawi,” msemaji wa polisi wa mkoa António Hossi ameeleza kwenye redio, akionya juu ya ongezeko la hivi karibuni la kesi hizi katika eneo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!