Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Urusi yafanya uchaguzi wa urais
Kimataifa

Urusi yafanya uchaguzi wa urais

Spread the love

Raia nchini Urusi kuanzia leo Ijumaa wanapiga kura katika uchaguzi wa urais utakaofanyika kwa siku tatu na unaotarajiwa kumuongezea muda zaidi, Rais Vladimir Putin. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Uchaguzi huo hata hivyo, unafanyika huku kukiwa na ukandamizaji mkubwa dhidi ya upinzani, vyombo huru vya habari na makundi maarufu vya haki za binadamu na kumfungulia mlango Putin wa kuudhibiti kikamilifu mfumo wa kisiasa.

Raia wanapiga kura kwenye vituo karibu 100,000 kuanzia hii leo Ijumaa hadi Jumapili ndani ya taifa hilo na kwenye maeneo yaliyonyakuliwa na Urusi huko nchini Ukraine katikati ya vita vilivyoingia mwaka wa tatu sasa.

Waangalizi hata hivyo hawatarajii kwamba uchaguzi utakuwa huru na haki kwa kuwa wapiga kura hawana uwanja mpana wa kuchagua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!