Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM, Daniel Godfrey Chongolo kuwa mkuu wa mkoa wa Songwe. Chongolo amechukua nafasi ya Dk. Fransis Michael ambaye amewekwa kando. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Chongolo aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza chini ya Raisi Samia Suluhu Hassan kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 alipojiuzulu, amewahi kuhudumu kama Mkurugenzi wa Mawasiliano chini ya Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ikiwa chini ya Nape Nnyauye.
Mwaka 2016 aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Loliondo. Mwaka 2018 akahamishiwa Kinondoni kwa wadhifa huo huo wa ukuu wa wilaya.
Chongolo amewahi kushika nafasi zingine kama vile Mhariri wa Radio Uhuru inayomilikiwa na CCM.
Leave a comment