Friday , 10 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja
Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the love

MWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, unatarajiwa kuzikwa tarehe 2 Machi 2024, mjini Unguja. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ratiba ya mazishi ya marehemu Mwinyi imetangazwa leo tarehe 29 Februari 2024 na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akitangaza kifo chake.

“Kwa niaba ya Serikali ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu. Nchi yetu itakuwa katika kipindi cha siku saba za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia kesho Machi 1, 2024,”  amesema Rais Samia na kuongeza:

” Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi atazikwa tarehe 2 Machi 2024 huko Unguja, kisiwani Zanzibar.

Inna Lillahi wa inna ilayhi raaji’un.”

Rais  Mwinyi,  amefariki dunia leo Ijumaa tarehe 29 Februari  2024 majira ya  saa 11:30 jioni, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Saratani ya Mapafu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Spread the loveKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

error: Content is protected !!