Mahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia, Moncef Marzouki kifungo cha miaka nane jela baada ya kupatikana na hatia kwa kutaka kuchochea fujo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Marzouki, ambaye alikuwa mkuu wa kwanza wa dola kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia baada ya vuguvugu la mapinduzi katika nchi za kiarabu mwaka 2011, anaishi nchini Ufaransa na hakuwepo mahakamani wakati hukumu hiyo ilipotolewa.
Msemaji wa mahakama amesema hukumu hiyo imetolewa kuzingatia kauli zilizotolewa na Marzouki zinazojumuisha uchochezi katika hotuba aliyoitoa mjini Paris.
Mwaka 2021 Marzouki ambaye aliiongoza Tunisia kuanzia mwaka 2011 hadi 2014, alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kutishia usalama wa taifa baada ya kuitaka Ufaransa isitishe msaada wake kwa rais wa Tunisia Kais Saied kwenye maandamano ya mjini Paris.
Leave a comment