Monday , 13 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Prof Muhongo ataka ubunifu mitaala mipya ya elimu
ElimuHabari za Siasa

Prof Muhongo ataka ubunifu mitaala mipya ya elimu

Wanafunzi darasani
Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuhakikisha  maarifa, ujuzi, uvumbuzi na udadisi vinazingatiwa kwenye mitaala mipya ya elimu ili kupata wahitimu watakaoweza kushindana katika soko la ajira la kimataifa hasa kwenye masuala ya sayansi na teknolojia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo ulitolewa jana tarehe 8 Februari 2024 na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, bungeni jijini Dodoma.

Prof. Sospeter Muhongo, Mbunge wa Musoma Vijijini

Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema ajira zenye uhitaji wa watu ulimwenguni ni zile zinazohusiana na masuala ya sayansi na teknolojia, ikiwemo za ukuzaji program (Software development), uchambuzi wa habari za kisayansi za data (Data scientific information analyst), uchambuzi na usimamizi wa akili bandia (Management analysis artificial intelgence) na uuguzi.

Amesema ili Serikali iandae watanzania watakaofanikiwa kuzipata kazi hizo ni lazima ibadilishe muundo wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), ili iwe taasisi badala ya tume.

“Nikiangalia ajira ambazo zinapatikana na kazi namba dunia inayotafuta watu ni software development na  manesi unajua COVID-19 walikufa wengi sana hivyo dunia wanatafuta manesi wenye uwezo, hizi ndizo kazi duniani ili tuzipate lazima na taasisi ya sayansi la sivyo hatutavuka,”amesema Prof. Muhongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!