Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania kunufaika na trilioni 14 za miradi Italia
Habari za Siasa

Tanzania kunufaika na trilioni 14 za miradi Italia

Spread the love

Tanzania imechaguliwa kuwa moja ya nchi nane za Afrika zitakazopewa kipaumbele na Italia kupitia mpango mpya wa kimkakati wa Mattei (Mattei Plan) ambapo kiasi cha  Euro bilioni tano (Sh 14 trilioni) za awali kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Miradi hiyo ya kipaumbele kupitia Mpango mpya wa Kimkakati wa Mattei (Mattei plan) ipo katika sekta ya nishati, elimu na kilimo.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumapili na Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Italia, Mhandisi Alfredo Cestari alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba pembezoni mwa Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaendelea Roma, Italia.

Mhandisi Cestari alieleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika na Italia, ambapo Serikali ya nchi hiyo itafadhili miradi ya kipaumbele kwa nchi nane za awali za Afrika. Hatua hiyo itahusisha pia kugharamia gharama za upembuzi yakinifu ya miradi itakayopendekezwa.

Katika utekelezaji ya mpango huo, ujumbe wa wataalam kutoka Chemba ya Biashara ya Italia ikiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Dk. Edmondo Cirielli unatarajiwa kuwasili nchini Tanzania ndani ya mwezi mmoja kwa ajili ya kukutana na timu ya wataalam ya upande wa Tanzania kwa ajili ya kukamilisha hatua za awali za utiaji saini wa ushirikiano huo wa pande mbili utakaohusisha utekelezaji wa miradi itakayopitishwa na pande mbili.

“Serikali ya Italia imetenga kiasi cha Euro bilioni 5 za awali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo katika nchi nane za kipaumbele za Afrika ikiwemo Tanzania,” alisema Mhandisi Cestari.

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ameipongeza Serikali ya Italia kwa kuonesha nia ya kuimarisha uhusiano wake na nchi za Afrika kupitia Mpango mpya wa Kimkakati wa Mattei (Mattei plan) ambapo sekta ya nishati, elimu na kilimo zimepewa kipaumbele.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umelenga kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili kupitia mpango mpya wa Mattei, (Mattei Plan).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!