Monday , 13 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Vita Gaza: Afrika Kusini yaishtaki Israel ICC
Kimataifa

Vita Gaza: Afrika Kusini yaishtaki Israel ICC

Spread the love

NCHI ya Afrika Kusini, imefungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ta Uhalifu wa Jinai (ICC), dhidi ya Israel ikiituhumu kwa kufanya mauaji ya kimbari kwenye eneo la Ukanda wa Gaza, nchini Palestina. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Baada ya Afrika Kusini kufungua kesi hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilikanusha juu ya madai hayo ikidai hatua hiyo inalenga kulichafua taifa lake.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, tayari Umoja wa Mataifa (UN), umethibitisha uwepo wa kesi hiyo inayoituhumu Israel kwa uvunjaji wa mkataba wa mauaji ya kimbari ambao imeuridhia.

Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, imesema wamefungua kesi hiyo ili kuzuia mauaji ya halaiki kuendelea kutokea kwa wananchi wa Gaza, baada ya kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas, kuingia vitani na majeshi ya Israel.

“Afrika Kusini inasikitishwa sana na hali mbaya ya raia walionaswa katika mashambulizi ya sasa ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza, kutokana na matumizi ya nguvu kiholela na kuwaondoa wakazi kwa nguvu,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza:

“Aidha, kuna ripoti zinazoendelea za uhalifu wa kimataifa, kama vile uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita, unaofanywa pamoja na ripoti kwamba vitendo vinavyokidhi kizingiti cha mauaji ya kimbari au uhalifu unaohusiana … vimefanywa na bado vinaweza kufanywa katika muktadha wa mauaji yanayoendelea Gaza.”

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kuunguruma wiki ijayo, ambapo Afrika Kusini inaiomba ICC itoe amri ya kuitaka Israel isistishe mara moja mapigano kwenye ukanda huo.

Vita kati ya Israel na Hamas, inaendelea kushika kasi tangu ilipoanza Oktoba mwaka huu, ambapo wapalestina zaidi ya 20,000 wameripotiwa kupoteza maisha.

Kwa upande wa Israel, raia zaidi ya 1,000 wamepoteza maisha ambapo wengi waliofariki katika shambulio la kushtukiza lililofanywa na Hamas tarehe 7 Oktoba 2023

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!