Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Samia:Bajeti ijayo tutazingatia ujenzi nyumba za walimu
Elimu

Samia:Bajeti ijayo tutazingatia ujenzi nyumba za walimu

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake inafanyia kazi changamoto ya upungufu wa walimu nchini, huku akiweka wazi mpango wake wa kutaka kuwajengea nyumba walioko kazini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi akizungumzia ziarani mkoani Singida,  leo tarehe 16 Oktoba 2023, amesema kwa sasa nchi inakabiliwa na upungufu wa asilimia 40 ya walimu wa shule ya msingi na asilimia 26 wa shule za sekondari.

“Suala hili tunakwenda kulifanyia kazi na nimearifiwa kuwepo uhitaji wa nyumba za walimu, hili tunalijua nataka niwahakikishie bajeti ya mwakani Serikali itajielekeza zaidi kwenye ujenzi wa nyumba za walimu. Tumeanza kujenga lakini ni kweli hazijatosha na walimu wanashindwa kukaa maeneo yao kutokana na upungufu wa nyumba,” amesema Rais Samia.

Akizungumzia maendeleo ya sekta ya elimu, Rais Samia amesema serikali yake inaendelea kupeleka fedha katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi pamoja na uendeshaji wa sera ya elimu bila malipo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

error: Content is protected !!