Friday , 10 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wasanii kitanzini, JWTZ yatoa siku 7 wanaovaa, kuuza sare za jeshi hilo
Habari Mchanganyiko

Wasanii kitanzini, JWTZ yatoa siku 7 wanaovaa, kuuza sare za jeshi hilo

Spread the love

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa muda wa siku saba kwa wananchi na wafanyabiashara nchini kusalimisha mavazi ya jeshi hilo au yale yanayofanana na sare za kijeshi. Anaripoti Anthony Sollo, Dodoma …(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 24 Agosti 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), Luteni Kanali Gaudentius Gervas Ilonda wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Amesema kuwa jeshi hilo limeshtushwa na kuwepo kwa wimbi kubwa la baadhi ya wananchi au kuonekana wamevaa sare za JWTZ ikiwemo mavazi yanayofanana na sare za kijeshi.

“Tumekutana hapa leo ili kupitia kwenu JWTZ litoe ufafanuzi kwa jamii ya Watanzania (wananchi) kuhusiana na kadhia hiyo inayokinzana na katazo la sheria linalokataza raia kuvaa kumiliki au kuuza mavazi ya kijeshi au yanayoelekea kufanana na sare za kijeshi” amesema Leteni Ilonda.

Luteni Ilonda amesema mavazi yanayokatazwa kuvaliwa ni pamoja na kombati (vazi la mabaka mabaka) makoti, tisheti, suruali, magauni, kofia, viatu, mabegi na kaptura zenye rangi zinazofanana au kushonwa katika mtindo ya kijeshi.

Akifafanua kuhusu katazo Luteni Ilonda amesema katazo hilo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 99 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) sura ya 192, Sheria namba 24 ya 1966 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

“Kifungu cha 178 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 (penal code) na Kifungu cha 6 cha Sheria ya Usalama wa Taifa vinakataza raia kuvaa sare na mavazi ya majeshi ya ulinzi au yanayofanana nayo.

“Wapo baadhi ya watu ambao kwa kutumia mavazi hayo wamekuwa wakiwatapeli wananchi huku wengine wakitumia kufanya vitendo vya kihalifu huku wakidhaniwa kuwa ni wanajeshi.

“Vitendo vya matumizi ya mavazi ya kijeshi ni uvunjifu wa sheria za nchi hivyo havipaswi kufumbiwa macho na hali hii ikiachwa kuendelea unaweza kuhatarisha Ulinzi na Usalama wa nchi yetu” amesema Luteni Ilonda.

Hata hivyo, Luteni Kanali Ilonda amesema kuwa zipo taasisi zinazowashonea watumishi wake sare za aina hiyo wakiwemo wafanyabiashara wanaoingiza nchini mavazi ya aina hiyo na kuyauza kwa baadhi ya raia kupitia katika maduka au maeneo yao ya biashara.

Katika hatua nyingine amewataka wasanii wanaovaa mavazi hayo na kuyatumia wawapo kwenye majukwaa ya kazi zao bila kufuata utaratibu wafuate sheria kwa kuomba vibali ili waweze kutumia mavazi na kwamba iwapo hawatatekeleza hatua kali zitachukuliwa.

Amesema JWTZ itaendelea kudumisha ushirikiano na mshikamano na wananchi ili kutimiza jukumu lake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kikokotoo na mafao vyatikisa Bunge, Spika ataka kibano kwa mifuko

Spread the loveSAKATA la kanuni mpya za ukokotoaji mafao ya wastaafu (kikokotoo)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Spread the loveKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

error: Content is protected !!