Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mabalozi mtegoni, Samia akerwa balozi aliyekataliwa kwa ugoigoi
Habari za SiasaTangulizi

Mabalozi mtegoni, Samia akerwa balozi aliyekataliwa kwa ugoigoi

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka mabalozi wapya aliowaapisha leo Jumatano kuelekea kwenye vituo vyao vya kazi wakiwa wamekamilika kwa sababu muda wowote wanaweza ‘kutumbuliwa’ baada ya kupokea ripoti ya tathmini ya utendaji kazi wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki. Anaripoti Mlelwa Kiwale (TURDACo)…(endelea).

Pia ameeleza kukerwa na mabalozi wasiojielewa kwa kuendekeza uvivu huku baadhi yao wakifanya kazi ya kupokea ujumbe wa wageni kutoka Tanzania, kuwapangia ratiba na kushughulikia watanzania wakorofi katika nchi wanazowakilisha.

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo tarehe 16 Agosti 2023 Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati akihutubia katika hafla ya kuwaapisha mabalozi wapya aliowapangia vituo vya kazi wiki iliyopita.

Baadhi ya mabalozi waliopishwa leo Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakimsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan

Amesema hivi karibu aliunda kamati maalumu ya kufanya tathmini kuhusu utendaji kazi wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ambayo imempelekea ripoti ya awali kuhusu kasoro na maboresho ya wizara hiyo.

Amesema baada ya kupokea ripoti hiyo, ameirejeshea kamati hiyo na kuitaka kuiboresha hivyo atakapopokea ripoti kamili muda wowote mabalozi hata hao wapya waliopishwa leo wanaweza kurejeshwa nyumbani au kuhamishwa.

“Baada ya kupata ripoti ya kamati mnaweza mkageuzwa tena, nenda jiaminishe nimewekwa hapa naanza kazi kiukwelikweli, hatutegemei sana mabadiliko lakini yanaweza kutokea,” amesema.

Aidha, ameeleza kukerwa na baadhi ya mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi walizopangiwa kwenda kustarehe na familia zao badala ya kufanya kazi zilizowapekeleka.

Ametoa mfano kuwa Rais mmoja wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), alimuomba balozi wa Tanzania arejeshwe kwa kuwa goigoi (mvivu) hashiriki hata mikutano inayofanyika katika nchi hiyo.

“Katika nchi nyingine mabalozi wetu hawajui wanachokifanya… wapo tu, nilishakutana na rais mwenzangu ndani ya SADC akaniambia ‘nibadilishie balozi uliyeniletea, maana hata kazini haendi, mikutano hashiriki yupoyupo tu hatumuelewi kwa sababu Watanzania hatuwajazoea hivyo labda ubadilishe’, nikamuambia nimekusikia” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!