Saturday , 18 May 2024
Home Kitengo Michezo Mamdonga atambulisha ngumi yake mpya sabasaba
Michezo

Mamdonga atambulisha ngumi yake mpya sabasaba

Spread the love

BONDIA machachari nchini Karim Said maarufu ‘Mandonga Mtu kazi’ ametembelea banda la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kutangaza ngumi mpya iitwayo “Kingugi” anayotarajia kuitumia kwenye mchezo wa marudiano na Bondia Daniel Wanyonyi kutoka Kenya.  Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mandonga ametangaza ngumi hiyo leo tarehe 29 Juni 2023 kwenye maonesho ya 47 ya Kimataifa Sabasaba ambayo yanaendelea jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

Mandonga ameishukuru Serikali kwa kusimamia vema michezo hatua iliyomfanya ajulikane kimataifa na kuhamasisha vijana kupenda michezo ili kuendesha maisha yao.

Akimkaribisha bondia Mandonga Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo ya 2023, Zahara Guga amesema Wizara ni mlezi wa masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hivyo, Mandonga ni miongoni mwa Wadau wake yupo kwenye ofisi yake ya kazi.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imejikita kutoa huduma kwa wananchi na wadau wa sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuhamasisha wadau hao kurasimisha kazi zao ambazo ni ajira ya kujipatia kipato kwa kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!