Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi 275 watumia darasa moja kusoma, Serikali yataja mikakati
Elimu

Wanafunzi 275 watumia darasa moja kusoma, Serikali yataja mikakati

Wanafunzi
Spread the love

KUTOKANA na uwepo wa msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule ya msingi Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe uliosababisha wanafunzi 270 kusomea katika darasa moja, Serikali inatarajia kutumia zaidi Sh 538 milioni kujenga shule pacha.

Aidha, kwa upande wa wazazi nao wamejitolea kuunga mkono juhudi hizo za serikali kwa kusafisha eneo litakalotumika kujenga shule mpya. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Akizungumza leo tarehe 28 Juni 2023, Samuel Mfune mkazi wa mtaa wa Isanzo Chapwa, amesema watoto wao wanashindwa kusoma vizuri kutokana na uhaba wa madarasa na wanakaa zaidi ya 270 badala ya 45 wanaotakiwa kusoma katika chumba kimoja hali inayosababisha ufaulu duni katika shule hiyo.

Mkuu wa shule hiyo, Jumanne Kibona amesema serikali imesikia kilio cha wananchi kwa kujenga shule pacha ya Isanzo kupunguza msongamano uliopo kwani darasa la tatu pekee wapo wanafunzi 275 wanasoma chumba kimoja badala ya 45.

Afisa elimu msingi wa halmashauri ya mji Tunduma, Caster Mbawala amesema karibu shule zote zina wanafunzi wengi lakini wanajitahidi kujenga shule mpya za ghorofa na za kawaida kukabiliana na idadi ya wanafunzi iliyopo na kwamba kinachohitajika ni ushirikiano kati ya wananchi na serikali katika kufanikisha mkakati huo.

Afisa mipango halmashauri ya mji Tunduma, Brown Garigo amesema gharama ya ujenzi wa shule hiyo ni Sh 538.5 milioni kutoka serikali kuu.

Amesema wananchi wamechangia nguvu kazi kwa kusafisha eneo la mradi panapojengwa shule na sasa ujenzi upo umefikia asilimia 65.

Amesema ujenzi huo ukikamilika utaondoa au kutapunguza tatizo la msongamano na huu ni mpango wa halmashauri.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ayoub Mlimba amesema serikali imesikia kilio cha wananchi ndipo maana imetoa kiasi hicho cha fedha kujenga shule pacha kupunguza msongamano.

Amesema idadi ya  watu Tunduma inaongezeka kila kukicha kwa kuwa mji ni kibiashara hivyo watu wengi wanaenda kuwekeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!