Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais wa zamani alaani mali zake kutwaliwa na utawala mpya
Kimataifa

Rais wa zamani alaani mali zake kutwaliwa na utawala mpya

Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu
Spread the love

WAKILI wa Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu, amelaani hatua ya serikali ya nchi hiyo, kutwaa mali mbalimbali zinazohusishwa na familia mwanasiasa huyo, na kusema kuwa kitendo hicho kimechochewa kisiasa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Rais wa sasa wa Zambia Hakainde Hichilema amekuwa akikabiliana na ufisadi, lakini wakosoaji wanasema analenga wapinzani wake wa kisiasa.

Serikali ilitwaa rasmi mali hizo kutoka kwa familia ya Lungu wiki iliyopita, ambazo ni pamoja majengo 15 ya ghorofa mbili kila moja, nyumba ya kulala wageni ya gorofa tatu, shamba na nyumba ya kawaida. Mali hizo zilichukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utaifishaji wa Mapato ya Uhalifu ya mwaka 2010, ambayo inaruhusu serikali kutwaa mali ambayo inaamini ilipatikana kwa njia zisizo halali.

Wakili wa Rais huyo wa zamani, Makebi Zulu, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba yeye wala wateja wake hawajapewa notisi ya mchakato wowote, ulio mbele ya mahakama yoyote kuhusu kukamatwa kwa mali hiyo.

Akizungumza na vyombo vya sheria tangu uchunguzi huo uanze mwaka jana, Zulu alisema wateja wake wametoa maelezo ya kutosha jinsi walivyopata mali hizo.

Alisema serikali inazuia kwa makusudi taarifa hizo ili kuwaaibisha Lungu, mke wake Esther Lungu, na watoto wao.

Wakosoaji wa Rais wanasema tangu serikali yake ilipoanza kuwakamata viongozi wa utawala uliopita na kuwafanyia uchunguzi wa madai ya vitendo vya rushwa, hakuna yeyote kati yao aliyepatikana na hatia yoyote.

Hichilema anasisitiza kuwa vita dhidi ya ufisadi havina maana ya kuwadhulumu wapinzani wake wa kisiasa.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!