Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vodacom, Tecno wazindua Camon 20 series, atakayenunua kuzawadiwa GB 96
Habari Mchanganyiko

Vodacom, Tecno wazindua Camon 20 series, atakayenunua kuzawadiwa GB 96

Spread the love


KAMPUNI ya Vodacom Tanzania ikishirikiana na Tecno Tanzania wamezindua simu mpya aina ya Tecno Camon 20 series iliyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Simu hiyo yenye uwezo mkubwa katika picha, kutunza chaji, imezinduliwa leo tarehe 20 Mei, 2023 jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa Vodacom, Samwel Mlelo amesema wana furaha kubwa kujumuika na Tecno Tanzania katika uzinduzi huo wa simu bora kabisa ambayo itasaidia kutimiza lengo lao kama Vodacom la kuhakikisha kila mtanzania anatumia simu bora.

“Vodacom ni zaidi ya kampuni ya simu, hivyo ina lengo la kuhakikisha kila mtanzania anatumia simu bora ambayo itamuwezesha kupata kile anachokitaka, kupitia Tecno Camon 20 series itakata kiu ya mtumiaji wa simu,” alisema Mlelo.

Mlelo alisema Vodacom itamzawadia kila atakayenunua Tecno Camon 20 atapata GB 96 za intaneti bure kwa mwaka mzima ikiwa ni GB 8 kwa kila mwezi.

“Ofa hii itamwezesha mnunuzi wq Tecno Camon 20 kupata GB 96 kwa muda wa mwaka mmoja ambapi ni sawa na GB 8 kwa kika mwezi kutoka Vodacom kwa miezi 12,” alisema Mlelo.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Masoko wa Tecno Tanzania, Salma Shafii amesema wanajuvunia kuzindua simu hiyo ambayo imefanyiwa maboresho makubwa kulingana na matakwa ya wateja wa Tecno.

“Simu hii imekuja na maboresho makubwa katika kamera yake, spidi na uwezo mkubwa wa kuhifadhi chaji,” alisema Salma.

Salma alisema simu ya Tecno Camon 20 series imekuwa na ubora mkubwa ambao umemshawishi msanii mkubwa wa Nigeria, Thiwa Savege ambaye kabla ya kukubali kuwa balozi wa simu hiyo baada ya kukagua ubora wake.

“Kama simu hii ya camon 20 imemshawishi msanii mkubwa barani Afrika, tunakushauri nawe mteja wetu wa Tecno ujaribu simu hii ambqyo tuna uhakika utaridhika na ubora wake,” alisema Salma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!