Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Maji yaendelea kusambazwa Musoma Vijijini
Habari Mchanganyiko

Maji yaendelea kusambazwa Musoma Vijijini

Spread the love

 

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), umeendelea kusambaza maji katika vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, miongoni mwa vijiji hivyo ni Bwasi, Bugunda na Kome, ambavyo usambazaji wake unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Taarifa hiyo imesema kuwa, jimbo la Musoma Vijijini lenye kata 21, lina miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa.

Mradi mmojawapo unaotekelezwa jimboni humo ni bomba la Bujaga-Bulinga-Busungu, linalotoa maji kutoka Ziwa Victoria.

“Tanki la ujazo wa Lita 200,000 limejengwa kijijini Busungu na lingine la Lita 150,000 limejengwa kijijini Bulinga. Maji kutoka kwenye matenki hayo ndiyo uanasambazwa kwenye vijiji vya Bukima na Kwikerege, gharama ya mradi ni Sh. 997,714,196” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“Shukrani za dhati zinatolewa kwa Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendeleza kusambaza maji safi na salama ya bomba Vijijini mwetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!