Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama yaagiza akaunti 15 za mchungaji mwenye utata Ezekiel Odero kuzuiliwa
Kimataifa

Mahakama yaagiza akaunti 15 za mchungaji mwenye utata Ezekiel Odero kuzuiliwa

Pastor Ezekiel Odero
Spread the love

 

AKAUNTI 15 zinazomilikiwa na Mchungaji mtata, Ezekiel Odero, zimeamriwa na Mahakama nchini Kenya kuzuiliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa zinasema, amri ya kuzuia akaunti hizo zilizopo kwenye mabenki tofauti, imekuka kufuatia ombi lililowasilishwa na Ofisi ya Mkurungenzi wa Mashitaka (DCI), mahakamani hapo jana.

Katika waraka uliowasilishwa mahakamani, DCI, ilidai kuwa Mchungaji huyo wa Kanisa la New Life Prayer Centre, anashukiwa kwa utakatishaji wa fedha.

Anatuhumiwa kuwa na uhusiano na Mchungaji wa Kanisa la Good News International, Paul Mackenzie, ambaye anachunguzwa kwa madai ya kuwalaghai wafuasi wa kanisa lake, kufunga hadi kufa ili ‘’kukutana na Yesu.”

Wapelelezi waliiambia Mahakama kuwa akaunti za benki za Mchungazji zimekuwa zikipokea kiasi kikubwa sana cha fedha ambazo zinashukiwa kuwa haramu.

Anasema, mamilioni hayo ya shilingi za Kenya na fedha nyingine za kigeni, zinatoka kwa wahanga ambao wanadaiwa kulaghaiwa kuuza mali zao na kumpatia mchungani Mackenzie.

Wameitaka mahakama kuwaruhusu kuzifikia akaunti kadhaa zilizopo katika mabenki ya Equity Co-op Bank, Kenya Commercial Bank (KCB) na Housing Finance Company Limited (HFC Bank).

Kulingana na afisa wa polisi waanayefanyia uchunguzi DCI, Martin Munene, Jamhuri inahofu kuwa fedha hizo zilizoshikiliwa katika akaunti mbali mbali za benki zitahamishwa iwapo Mahakama haitatoa agizo la kuzifikia akaunti hizo.

Wiki iliyopita, mchungaji Ezekiel alikwenda katika Mahakama ya juu zaidi mjini Mombasa, akitaka kuzuia kufujwa kwa akauntu zake.

Alikuwa amedai kuwa kushikiliwa kwa akaunti zake kutakuwa ni kuingilia uhuru wake na wa kanisa, pamoja na waumini wa kanisa analoliongoza.

Suala hilo linatarajiwa kuendelea kusikilizwa mahakamni kesho Jumanne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!