Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Raia 200 wa Tanzania waliokwama Sudan kurejea nchini
Habari za Siasa

Raia 200 wa Tanzania waliokwama Sudan kurejea nchini

Dk. Stergomena Tax
Spread the love

 

SERIKALI imesema kuwa Watanzania 200 waliokwama nchini Sudan wakati huu ambako taifa hilo likiwa kwenye machafuko wapo njiani kurejea nyumbani. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam …(endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Aprili 2022 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Lawrence Tax, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dk. Tax amesema kuwa Serikali ikishirikiana na Bolozi za Jamhuri ya Sudan na Ethiopia imetumia fursa ya makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano kwa siku tatu kuanzi tarehe 21 mpaka 23 Aprili, kuondosha raia wa kigeni ili kurejea katika nchi zao.

Amesema kuwa Watanzania hao waliofika katika mpaka wa Ethiopia kwa ajili ya kuelekea kwenye mji wa Adis Ababa kwa lengo kusafiri ambapo tayari ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), inawasubiri kuwarejesha nchini.

“Leo wamefika mpakani na Ethiopia na wakifika huko watakuta ndege ya Air Tanzania inawasubiri kuwarudisha Tanzania,” amesema Dk Tax.

Aliongeza kuwa serikali imeona haja ya kuwasaidia raia pia wa ya Uganda, Kenya Burundi ,Zimbabwe,Msumbiji wakiwa kwenye safari moja.

Hata hivyo, baadhi ya raia wa Kenya, tayari wameondolewa nchini Sudan kwa ndege ya jeshi, kutokea uwanja wa ndege wa taifa la Sudan ya Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali jijini Nairobi, msafara mwingine wa raia wa taifa hilo, Unatarajia kufanyika kesho, ambako mamia ya wananchi wanatarajiwa kusafirishwa kutoka Sudan kuelekea Kenya.

Dk. Tax amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kutoa maelekezo ya maofisa wa kidiplomasia juu ya safari hiyo “muda wowote tutawapokea ndugu zetu watawasili nchini.”

Imeripotiwa zaidi ya watu 400 wameuawa na wengine 3,500 , wamejeruhiwa kwenye mapigano hayo yanayohusisha kikosi cha Rapid Support Force (RSF) na jeshi la serikali .

Wakati huo huo Dk. Tax amekiri kuwa kundi la Waasi la Oromo la nchini Ethiopia wametua nchini Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya kusitisha mapigano nchini mwao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!