Tuesday , 14 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Lori laparamia na kuua madereva bodaboda 10
Kimataifa

Lori laparamia na kuua madereva bodaboda 10

Spread the love

WATU 10 wanadaiwa kupoteza maisha baada ya lori lililokuwa likisafirisha changarawe kupoteza mwelekeo na kuparamia kijiwe cha bodaboda katika eneo lao mjini Migori nchini Kenya. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea leo tarehe 8 Aprili 2023, inaelezwa ni vijana wa bodaboda waliokuwa wakisubiria wateja kwenye kijiwe chao.

Umati mkubwa wa watu ulimiminika eneo la tukio ili kuwanusuru majeruhi na kuwakimbiza hospitalini kwa matibabu.

Kwa mujibu wa raia mmoja aliyeshuhudia na kuzungumza na runinga ya TV47, breki za lori hilo zilifeli na kuingia katika kundi hilo la bodaboda ambao walikuwa wanasubiri abiria.

Ajali hiyo imetokea karibu na shule ya msingi ya Migori. Eneo la tukio lilikuwa limejaa damu na miili. Vyuma pia vilikuwa vimetapakaa eneo hilo.

Eneo la tukio linaripotiwa kuwa na zaidi ya miili 10 huku gari za kubeba wagonjwa ‘ambulansi’ na zima moto kutoka kwa serikali ya kaunti ya Migori zikifika eneo la ajali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!