RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imeonyesha mikopo yenye thamani ya Sh milioni 167 haijarejeshwa na wafanyakazi katika Mamlaka ya Elimu Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Ripoti hiyo ya mwaka wa fedha 2021/2022 iliyowasilishwa bungeni juzi tarehe 6 Aprili 2023 jijini Dodoma, ilisema maofisa 10 wanadaiwa shilingi milioni 167 kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja hadi 10 bila ya mpango madhubuti wa kurejesha mikopo hiyo.
Imesema mikopo hiyo imebaki bila kulipwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uhamisho na kustaafu kwa maofisa.
Hata hivyo, imesema uongozi ulieleza kuwa hatua zaidi zimepangwa kuchukuliwa ili kurejesha mkopo uliobaki ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kisheria.
“Kwa maoni yangu, ikiwa mikopo haitarudishwa kwa wakati, Mamlaka itapata hasara. Ninapendekeza Mamlaka ya Elimu Tanzania ichukue hatua stahiki katika kukusanya mikopo iliyosalia ya wafanyakazi,” imesema ripoti hiyo.
Leave a comment