Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mpango wa Ukraine, Marekani na NATO kushambulia Urusi wavuja kwenye mitandao ya kijamii
Kimataifa

Mpango wa Ukraine, Marekani na NATO kushambulia Urusi wavuja kwenye mitandao ya kijamii

Spread the love

 

PICHA za hati za siri kutoka Pentagon na NATO juu ya utayarishaji wa shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi zimevuja katika mitandao ya Twitter na Telegraph. Yameripoti Mashirika ya Kimataifa…(endelea).

Licha ya kuonekana kubadilishwa kiasi hati hizo zinaonekana kuwa za kweli kulingana na gazeti la New York Times, likinukuu vyanzo visivyojulikana katika utawala wa Biden.

Tarehe za hati hizo ilikuwa Machi Mosi , hivyobasi inakisiwa kwamba huenda mipango inaweza kuwa ilibadilika tangu wakati huo.

Hata hivyo hazitaji eneo au mahala pa mashambulizi hayo.

Lakini zina habari kuhusu brigedi ngapi Ukraine inapanga kujiandaa kwa shambulio hilo na ni vifaa gani watapata na kutumia wakati huo. Pia wana taarifa kama vile matumizi ya kila siku ya risasi kwa HIMARS.

Ukweli kwamba nyaraka zingeweza kubadilishwa unathibitishwa na ukweli kwamba kwenye moja ya hati hizo, hasara iliopata wanajeshi wa Urusi inakadiriwa kufikia kati ya 16-17,000, huku Ukraine ikiwa 71.5 elfu, kwa mujibu wa gazeti hilo.

1 Comment

  • Warusi kati ya 16-17, 000 na waukraine 71,500? Duh!
    Zile ndege za F-16 zinaogopa makombora ya supersonic? Duh!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!