Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DPP awafutia mashtaka ya ugaidi Masheikhe 36
Habari Mchanganyiko

DPP awafutia mashtaka ya ugaidi Masheikhe 36

Spread the love

 

MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, amewafutia mashtaka waislamu waliokuwa wanakabiliwa na makosa ya ugaidi ikiwemo Masheikh, katika mahakama mbalimbali nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 21 Februari 2023 na Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania, Ibrahim Mkondo, DPP amefuta mashtaka hayo katika nyakati tofauti kuanzia tarehe 15 Februari mwaka huu.

Taarifa ya Mkondo imesema kuwa, tarehe 15 Februari 2023, DPP Mwakitalu aliwafutia mashtaka waislamu 17 waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.

Wasilamu nane kati ya 17, wameachwa huru kutoka mahabusu baada ya kukamilisha taratibu za kisheria, akiwemo Abdallah Issa Ramadhan, Abdallah Musa Fundi, Abdu Yusuf Nambungwa na Said Salum.

Taarifa hiyo imesema kuwa, tarehe 16 Februari 2023, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iliwafutia mashtaka ya ugaidi watu 16, ambapo mmoja ameachwa huru tarehe 20 Februari mwaka huu, baada ya kukamilisha taratibu za kisheria.

“Wenzao waliofutiwa mashtaka na bado wapo gerezani taratibu za kuwatoa zinaendelea kufanyika,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa ya Mkondo imesema licha ya watu hao kufutiwa mashtaka lakini bado kuna mamia ya waislamu walioshtakiwa kwa ugaidi, wako mahabusu za magereza mbalimbali nchini.

“Watuhumiwa hawa ni kati ya mamia ya Waislamu wanaosota gerezani kwa
muda mrefu wakiwemo waliofikisha miaka 10 baadhi yao ni viongozi wa dini, wanawake, watoto na wazee. Mzee Suleiman Ulatule mwenye umri wa miaka96,na familia yake ya watu sita, ni miongoni mwa watu hao wanaosota gerezani kwa muda mrefu,” imesema taarifa ya Mkondo.

Inadaiwa kuwa, sababu za watu hao kukaa gerezani kwa miaka mingi ni upande wa serika kushindwa kupeleka ushahidi dhidi yao.

“Tunashauri serikali iendelee kusimamia haki za watu wake na si kwa Waislam
pekee walioweka magerezani kwa muda mrefu, bali kwa mtu yeyote bila kujali
rangi, dini, kabila wala ukoo wake,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“Kama ambavyo Ofisi ya Muendesha Mashtaka (DPP), ilivyopitia na kuona
waliokuwa watuhumiwa hawana makosa waliyoshtakiwa na kuamua kuwaacha huru, tuna imani mchakato huu utaendelea kwa washtakiwa wengine ambao bado wanaendelea kukaa gerezani mpaka sasa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

error: Content is protected !!