Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi watakiwa kujiamini
Elimu

Wanafunzi watakiwa kujiamini

Spread the love

MKURUGENZI wa Shule za Feza Tanzania, Ibrahim Yunus amewataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini kujiamini wanaposhiriki midahalo ya kitaifa na kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Yunus amesema hayo wakati akifungua mashindano ya African Open School Debate yaliyohusisha shule 18 za serikali na binafsi ambayo yanafanyika kwa muda wa siku tatu ndani ya Shule ya Kimataifa Feza

Amesema shule zipatazo 18 zimeshiriki mashindano hayo za serikali na binafsi lengo ni kuwajenga wanafunzi waweze kujiamini kwenye midahalo mikubwa ya kimataifa na ya kitaifa na kuweza kujifunza vitu tofauti ambavyo vinaweza kujenga nchi na kutengeneza ushirikiano bora kwa wanafunzi katika masomo.

Naye Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kondo, Grace Saware amesema midahalo hii inawajenga watoto kwa asilimia kubwa kwa kuwa mada zinazotolewa ni nzuri ambazo zipo kwenye mitaala ya elimu ya hapa Tanzania.

Pia ametoa wito kwa serikalo kutengeneza program za midahalo ya shule za serikali katika wilaya, kata, na mkoa kwani zinawajengea uwezo mkubwa wanafunzi kujiamini na kujieleza hata kwenye mithihan yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!